September 14, 2015

Mgombea Urais Aangua Kilio Jukwaani Kisa Jakaya Kikwete

Jakaya Kikwete
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha Chauma, Mohammed Masod Rashid, amejikuta akiangua kilio jukwaani na kumpigia magoti Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, kumuomba awaachie huru masheikh wa Jumuiya ya Mihadhara ya Dini ya Kiislamu (Uamsho) waliopo gerezani.

Tukio hilo lilitokea katika mkutano wa hadhara wakati akifungua kampeni za chama hicho visiwani hapa.
Mgombea huyo alivuta hisia za wananchi na kila aliyekuwa akipita njia katika eneo hilo la kiwanja cha Komba Wapya kilichopo mjini hapa kusitisha safari yake na kuanza kumsikiliza wakati akiangua kilio.

Mgombea huyo aliacha kunadi sera na kuangua kilio akiwalilia masheikh hao wanaokabiliwa na kesi ya kusaidia ugaidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Nakupigia magoti Rais Kikwete naomba uwatoe masheikh wetu kwani unawavunjia haki zao za msingi, alisema mgombea huyo wa urais.
Alisema endapo atapata ridhaa ya Wazanzibari kuwa rais atatoa msamaha kwa wafungwa walioko gerezani ambao wanamakosa madogo madogo.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment