Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kuninusuru kifo, mimi na rafiki zangu katika ajali mbaya ya gari letu kugongwa na Fuso, Septemba 8, mwaka huu maeneo ya Bondeni, Mbezi-Beach jijini Dar.
Hakika Mungu ana kusudi na mimi katika kukuelimisha wewe msomaji wangu wa XXLove. Nanyi nawatakia afya njema, rafiki zangu waliojeruhiwa zaidi yangu katika gari tuliyopata nalo ajali naamini tumenusurika kifo.
Wiki iliyopita tulijifunza namna ya kurudisha uhusiano wako uliopotea au penzi lililopoteza mvuto au kuchuja. Leo tunaendelea kujifunza zaidi namna ambavyo unaweza kurudisha uhusiano wako kama ifuatavyo;

BADILIKA
Lazima ufike wakati uanze kubadilika, anza kuepuka makosa ambayo yamekuwa yakimkwaza mwenza wako au yakisababisha mtafaruku kwenye uhusiano wako. Kwa kufanya hivyo, uhusiano wako utaendelea kuwa thabiti kila siku.

UAMUZI
Suala la kubadilika ni uamuzi wako, katika moja ya vitabu vitakatifu kinamtaja Sauli kama mtu aliyeua na kuwatesa wana wa Mungu pamoja na kufanya kila aina ya maovu kiasi cha kumchukiza sana Mungu. Lakini mwisho wa siku mtu huyo aliamua kubadilika na kuwa mfano mzuri kiasi cha kuitwa mtume.

Si mwingine, namzungumzia Mtume Paulo, mmoja wa mitume aliyeandika vitabu vingi katika Agano Jipya kwenye Biblia.
OMBA MSAMAHA
Hata vitabu vitakatifu vinatutaka kumuomba Mungu msamaha, tena yeye akasema atatusamehe saba mara sabini, sasa kwa nini wewe mwanadamu usiombe msamaha kwa mwenza wako uliyemkosea mara mbili au tatu na kuendelea na yeye akakusamehe?

JUTIA
Onesha ni kwa namna gani unajutia yote yaliyokufanya au uliyofanya ukakosana na mwenza wako. Onesha kuchukia sababu hizo kuanzia usoni hadi moyoni mwako.

ANZA MAISHA MAPYA
Baada ya kulumbana na kukwazana na mwenza wako kwa muda mrefu, sasa anza maisha mapya. Cha msingi ni kukubali ulichokifanya na kuamini maisha yako au uhusiano mzuri unatengenezwa na wewe mwenyewe.

NDIYO MAISHA YAKO
Napenda uamini hayo ndiyo maisha yako halisi, hakuna maisha mengine, cha muhimu ni kuangalia namna gani ya kuyaboresha ili kudumu, kwani unaweza kuhisi mwenza wako ni mtukutu, dhaifu, mzinzi, mlevi na mengineyo kisha ukahamia kwa mwenza mwingine kwa kuamini yeye ni bora zaidi ya uliyemuacha, kumbe pasipo kujua yeye ndiyo majanga zaidi.

USIBABAISHWE NA MICHEPUKO
Kuna baadhi ya wapenzi wanababaika na michepuko na kusahau thamani kubwa waliyopewa na wenza wao kwa kupewa nafasi ya kuishi nao.

KWA NINI WENGINE WAMEDUMU
Suala la kujiuliza, mbona kuna watu wengine wako kwenye uhusiano, uwe wa ndoa, mapenzi au urafiki na wamedumu kwa miaka zaidi ya 10 na kuendelea? Nimpongeze msomaji wangu aliyejitambulisha kama baba Kelly wa Tunduma kwa kudumu kwenye ndoa na mkewe kwa miaka 21. Mungu awazidishie upendo, uvumilivu na busara katika kutatua migogoro yenu.

Usikose wiki ijayo kwenye mada nyingine tamu. Pia usikose kutembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Facebook kwa ushauri na maswali kuhusu uhusiano.
No comments:
Post a Comment