Na Fred Bundala,Bongo5
Hii ni mara ya kwanza nakutana na Lady Jaydee
na kumfanyia interview ndefu. Kwangu
nimeichukulia kama heshima kubwa kwa
mwanamuziki huyu mkongwe kuamua kutafuta
muda na kuja kuchill na mimi.
Kabla sijaanza kuongea naye, namuambia Lady
Jaydee kuwa hii itakuwa interview ‘positive’ zaidi
kuwahi kuifanya katika miaka ya hivi karibuni.
“Sisi kwetu tumezaliwa watoto kumi,” anasema
Jaydee. “Lakini bahati mbaya watatu wamefariki
na tumebakia saba. Familia yetu ni familia ya dini,
tumezaliwa kwenye maadili ya kisabato,
tumekulia kanisani na nidhamu.”
“Nilikuwa naimba kwaya kanisani, nilishiriki pia
kwenye vikundi vya Pathfinder kanisani kwetu
tangu nina miaka saba yaani nilikuwa naweza
nikasimama mbele ya kanisa nikaongoza watu,
nikaimbisha watu wakaimba.
"Unajua ukiwa mdogo huwezi ukajua kama ni
kipaji, mimi nikawa naona ni kitu tu ambacho
napenda, kwahiyo nikawa nafanya tu for fun.”
Jaydee anasema alikuwa ni mtoto msikivu na
aliyekuwa akifuata kile alichokuwa akielekezwa na
wakubwa zake. “Muda mwingi nilikuwa nautumia
kanisani zaidi, kwahiyo ilikuwa ni shule,
kanisani,” anakumbuka.
Anasema tangu alipojitambua, muziki kilikuwa ni
kitu alichopenda kuja kukifanya kama kazi yake.
“Nilikuwa napenda kuwaangalia watu ambao
wanaimba na kujiweka kwenye viatu vyao na
kujifikiria vipi mimi nikiwa kama yule, sikuwa
najiona mtu mwingine zaidi ya mwanamuziki.”
Lady Jaydee alizaliwa mkoani Shinyanga hadi
darasa la nne kabla ya kuhamia jijini Dar es
Salaam. Akiwa Dar es Salaam, pamoja na kuwa
na ndoto ya kuja kuwa mwanamuziki, alijikuta
katika wakati mmoja akifanya kazi kama
mtangazaji wa redio.
“Saa zingine nilikuwa najaribu kutangaza TV
kwahiyo nakaa kwenye kioo najiangalia najaribu
kuona kama naweza kuwa presenter.
"Kwahivyo nikasema ngoja nikajaribu kuomba
labda kwenye redio pia nione kama ntaweza,
lakini mwenyewe binafsi siamini kama ni
mtangazaji.
"Ila nafikiri nilikuwa naenda kwasababu napenda
muziki na naona ndio sehemu ambayo naweza
nikakutana na watu ambao tunaweza tukafanya
masuala hayo ya muziki na vitu kama hivyo.”
“Nilifanya ile kazi lakini sio kwamba nilikuwa
naipenda sana kwasababu sio passion yangu.
Baadaye nilipoweza kufanya muziki nikaona
siwezi kuendelea na kitu ambacho hakipo kwenye
moyo wangu, nikaona nifanye muziki na niache
kutangaza.”
Wimbo wa kwanza Lady Jaydee kurekodi uliitwa
‘Sema Unachotaka’ aliourekodi kwenye studio za
Master J baada ya kushinda shindano
lililoandaliwa na Radio One Stereo.
Wimbo huo uliwekwa kwenye album iitwayo
Asubuhi iliyokuwa na nyimbo za wasanii wengine
pia.
Album yake ya kwanza ilikuwa ni Machozi
iliyokuwa na nyimbo nyingi za huzuni na
kuumiza japo anasema hiyo haikuashiria kuwa
hayo ndio yalikuwa maisha yake.
Kabla ya kuwa na jina, Jaydee alikuwa akirap na
Dr. Dre ambaye hadi leo ni role model wake,
alikuwa mmoja wasanii aliokuwa akiwasikiliza
sana. Ndoto yake hadi leo ni kuja kurekodi na
producer huyo.
“Siku zote tu nimekuwa nikiwish tu kwamba labda
kama angeweza kunitengenezea hata wimbo
mmoja,” anasema Jaydee.
Maisha ya umaarufu yamekuwa na changamoto
nyingi kwake ikiwemo kujizuia kufanya mambo
anayoyapenda ambayo kama asingekuwa staa
angeyafurahia kuyafanya.
“Watu wanashindwa kuelewa kwamba mimi ni
Jaydee sawa lakini mimi ni Judith na ni binadamu
wa kawaida.” anasisitiza.
“Naweza kukasirika, naweza kucheka, naweza
kulia, naumia kama mtu mwingine anavyoumia.
Lakini wao wanavyochukulia ni kwamba
unavyokuwa pale wanapokuwa
wameshakufahamu, hutakiwi vitu vingine kufanya
kwahiyo unakuwa saa zingine hauko huru sana.
"Labda mtu amekuja amekuchokoza inabidi
umwache tu hauwezi kumrudishia wakati katika
hali ya kawaida mtu yeyote anaweza kufight
back.
"Na mimi ni mgomvi sana na huwa sipendi
kuonewa, saa zingine unaweza kukuta mtu
akakufanyia kitu lakini ukakaa tu kimya, huyo sio
mimi lakini inabidi tu nifanye hivyo.”
No comments:
Post a Comment