April 6, 2015

BREAKING NEWS ...POLISI AJIUWA KWA KUJIPIGA RISASI KICHWANI.....



POLISI AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI

Askari wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, H 3416 PC Charles, amejiua kwa kujipiga risasi.Baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na kituo hicho cha polisi, Paulo Lazaro na Furahisha Felix, walisema tukio hilo lilitokea Aprili 4, mwaka huu, saa 1:00 usiku kituoni hapo.“Suala hili limetushangaza, kwani sisi tulikuwa nyumbani. Ghafla tulisikia mlio wa bunduki katika kituo cha polisi. Tulipofika, tulimkuta askari huyo akiwa amekufa kwa kujipiga risasi,” alisema Lazaro.

Unadhani nini kinaweza kumpa mtu ujasiri wa kujiua?

No comments:

Post a Comment