March 1, 2015

Top Ten ya Mastaa wa Bongo Ambao Kuvaa Nusu Utupu Sio Ishu Kwao

Ukifuatilia sana kwenye nchi za wenzetu kama vile Marekani na kwingineko, mastaa hawako makini na suala la uvaaji. Yaani si ajabu kuona staa mkubwa akikatiza mtaani akiwa amevaa nguo ya ndani na ukishangaa utaonekana mshamba.

Wanaovaa hivyo hawajakosa nguo za heshima za kuvaa bali ni ule ulimbukeni wa kutaka wawe gumzo na kuendelea kuwa maarufu.Kutokana na athari ya utandawazi, hapa Bongo wapo mastaa ambao nao wameiga kiasi cha kutoona aibu kuvaa nguo zinazoacha wazi maungo yao.Najua wapo wengi lakini leo nimeona nikupe kumi bora ya mastaa hao.

Baby Joseph Madaha
Huyu ni mwanamuziki na muigizaji. Wengi wanamfahamu kwa kupenda kuyaacha wazi matiti yake sambamba na kupenda kuvaa visketi na vigauni vinavyoacha wazi sehemu kubwa ya mapaja.
Stejini ndiyo kabisa hadi kufuli lake kama siku hiyo amelivaa haoni aibu kulifanya lionekane kwa mashabiki wanaofuatilia shoo yake. 

Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’
Ni muigizaji aliyejaribu kuingia kwenye muziki lakini akashindwa. Naye ni kati ya mastaa wasiothamini miili yao. Ni mrefu kwa umbo lakini cha ajabu hupendelea kuvaa vipensi na visketi vifupi huku naye akiona poa watu kuona nido zake.

Tamrina Poshi ‘Amanda’
Kwa umbile wengi tunamjua kuwa ni kati ya mastaa waliofungashia ile mbaya. Hata hivyo, anatajwa kuwa miongoni mwa mastaa wa kike ambao hupenda kuwarusha roho wanaume akatizapo mtaani.
Kutokana na hilo, yeye ni muumini wa kutoanika nido zake lakini hupendelea kuvaa vigauni vifupi sana ambavyo wakati mwingine hata akitakiwa kuinama kuokota kitu hawezi, akiinama lazina kalio lake lote litabaki nje.

Isabella Mpanda ‘Bella’
Huyu ni kati ya mastaa mcharuko ambaye ni mama wa mtoto mmoja lakini linapokuja suala la kuvaa, mara nyingi hupenda kuvaa vinguo vifupi licha ya kwamba kimwili chake ni kidogo.

Jokate Mwegelo
Huyu havumi lakini yumo! Ni mwanamitindo ambaye ukimkuta kwenye sherehe za heshima huwezi kuamini kama ndiyo yule ambaye maeneo mengi yenye mkusanyiko wa watu huvaa vinguo vya kimitego.Kuona mapaja yake wala siyo ishu kwani kuna wakati huvaa vigauni vifupi sana au mashati makubwa bila suruali wala pensi. Hata hivyo, kuona nido zake ni shughuli.

Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’
Nani asiyemjua huyu kwa vurugu zake? Naye ana wowowo kama Amanda. Ingekuwa ni mtu anayejiheshimu angekuwa ni wa kuvaa madira na magauni makubwa lakini kwa mcharuko wake, yeye ni mwendo wa nguo fupi tu. Hata linapokuja suala la sehemu ya kifua, mara nyingi haoni hatari kuyaanika matiti yake.

Vanessa Mdee ‘V- Money’
Huyu ni Mtangazaji wa Radio Choice FM ya jijini Dar anayefanya vizuri kwenye muziki. Ukimfuatilia sana utagundua ni binti anayependa sana kuvaa vipensi na wakati mwingine fulana tu ambazo hufunika sehemu ndogo ya mapaja. Awapo stejini ndiyo usiseme. Huwa anapendelea kuvaa sidiria na visketi ambavyo akionesha manjonjo yake, kama kavaa kufuli lazima lionekane.


Aunt Ezekiel
Kwa sasa ni mjamzito lakini kutokana na kasumba yake bado utamkuta kavaa kipensi. Kwenye mitoko yake mara chache sana utamkuta kavaa kiheshima. Kwa wale wanaojua katalogi zake akiwa viwanja watakubalinana na mimi kwamba, ni binti ambaye haoni hatari wanaume ‘kumchungulia’.

Zuena Mohammed ‘Shilole’
Naye kajaaliwa kuwa na kijungu flani hivi. Ni staa wa muziki na filamu ambaye inavyoonekana kuvaa nguo za heshima kwake ni mwiko, labda awe amealikwa kwenye ‘minuso’ ya watu wenye heshima zao.

Lungi Maulanga
Huyu ni msanii wa filamu ambaye linapokuja suala la kuvaa kiheshima huenda mkagombana. Akiwa viwanja utamjua kuwa ni binti wa mjini asiyependa kujibanabana.
 Kwa kifupi anapenda kuvaa nguo za kihasara.
<<<<HILI NDILO NENO LA MWISHO ALILOSEMA KAPTENI ..KOMBA DAKIKA CHACHE KABLA YA KUFARIKI..>>

No comments:

Post a Comment