Musa Mateja
MREMBO kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Winfrida Josephat ‘Recho’, amepiga mwereka wa aina yake baada ya kuteleza ukumbini, Risasi Jumamosi limeshuhudia.
Tukio hilo lilijiri juzikati katika Hoteli ya Regence, Mikocheni jijini Dar ambapo mrembo huyo alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa (bethidei).
Wakati sherehe ikipamba moto, wageni waalikwa walimmwagia Recho maji na mvinyo kama ishara ya upendo na kusababisha sehemu aliyokuwa amekaa kutapakaa maji.
Wakati zoezi la kummwagia maji na mvinyo likiendelea, katikati ya sherehe, mwanahabari wetu aliyekuwepo ukumbini hapo, alishuhudia mrembo huyo akiteleza na kuanguka chini ambapo wenzake hao hawakujali, wakaendelea kummwagia hali iliyosababisha msanii huyo aangue kilio.
“Jamani inatosha, muoneeni huruma kidogo hii sasa si sherehe tena hapa mnamsulubu,” alisikika mmoja wa waalikwa.
Baadaye wageni waalikwa walimfuta Recho maji na zoezi la kukata keki na kulishana kwa ‘staili ya njiwa’ likaendelea huku waalikwa wakiendelea kukata ulabu.
Baada ya shamrashamra kutulia, mwanahabari wetu alimvuta pembeni Recho na kutaka azungumzie sherehe hiyo ambayo katikati ilimfanya aangue kilio: “Nimejikuta tu nikilia na hasa sikutegemea kama wangenimwagia pombe na maji kiasi kile, nywele nilizoweka kichwani zinaniuma sana lakini pia pombe ziliniingia machoni, kimsingi ni jambo la furaha lakini ndiyo hivyo limeniliza,” alisema Recho.
Sherehe hiyo iliwakusanya waalikwa mbalimbali akiwemo shosti yake Recho wa damu, staa wa Bongo Fleva, Esterlina Sanga ‘Linnah’.<<<<HILI NDILO NENO LA MWISHO ALILOSEMA KAPTENI ..KOMBA DAKIKA CHACHE KABLA YA KUFARIKI..>>
March 1, 2015
RECHO APIGA MWEREKA KATIKATI YA SHEREHE
Tags
# LIFE STYLE
# UDAKU
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
UDAKU
Labels:
LIFE STYLE,
UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment