MWANDISHI WETU
Tajiri anayetajwa kuwa na maduka kadhaa ya nguo sehemu mbalimbali jijini Dar, anayejulikana kwa jina la Mark Edi, ambaye inadaiwa yupo katika mipango ya kumuoa diva wa filamu nchini, Wastara Juma, amenaswa.
Chanzo makini kilicho karibu na wawili hao, kimelitonya gazeti hili kuwa mwanaume huyo amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na muigizaji huyo kwa muda mrefu na wakati wowote wanatarajia kufunga ndoa.
“Huyo Bond anayetajwa kuwa ndiye mtu wa Wastara ni kama geresha tu, mtu mwenyewe yupo na amejituliza. Na hata hivi karibuni iliporipotiwa kwamba alipoteza fahamu, ni kwa sababu ya mwanaume huyu, siyo huyo muigizaji mwenzake,” kilisema chanzo hicho huku kikilionyesha gazeti hili picha za wawili hao wakiwa wamepozi.
Gazeti hili lilifanikiwa kumpata Mark na lilipomuuliza kuhusu madai hayo, alikiri kuwa na uhusiano na mcheza filamu huyo, lakini akatahadharisha kuwa hata hivyo haikuwa ‘official’.
“Nafikiri muda ukifika kila kitu kitakuwa wazi, kwa sasa kuna mambo flani ninakamilisha halafu tutaweka hadharani. Kuhusu kukorofishana ni kweli kulitokea hitilafu kidogo, lakini tumeshaweka mambo sawa,” alisema Mark.
Jitihada za kumtafuta Wastara zilishindikana kwani simu yake ya mkononi ilikuwa haipatikani kwa muda wote aliopigiwa.
<<<<HILI NDILO NENO LA MWISHO ALILOSEMA KAPTENI ..KOMBA DAKIKA CHACHE KABLA YA KUFARIKI..>>>>>
No comments:
Post a Comment