Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Jakaya Mrisho Kikwete, akiongoza maelfu ya Watanzania kuuaga mwili wa Kapteni John Komba, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania Ali Hassani Mwinyi akipita kando ya jeneza lenye mwili wa John Komba.
Mkuu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi, Selemani Kova, akipiga saluti wakati wa kuaga.
Mwakilishi wa Kambi ya Upinzani, Joshua Nasari, wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)akiongea jambo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye (katikati) akiimba wimbo maalum na wasanii wa muziki wa dansi.
Rais Kikwete (katikati) akiwa na makamu wake Gharib Bilal (kushoto) na Spika Anna Makinda.
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa (wa pili kulia) akiwa na mkewe Anna (wa tatu kulia) wakiwasili viwanja vya Karimjee.
Waziri mkuu aliyejiuzulu,Edward Lowassa (kulia)akisalimiana na Mkapa.
Spika wa Bunge, Anna Mkapa (kushoto) akiwa na Mkapa.
Mbunge wa Kinondoni Idd Azzan (kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba (kulia) akiwa viwanja vya Karimjee.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (kulia)akisalimiana na mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale.
Wake wa marehemu Komba, katikati ni mke mkubwa, Salome, na kulia ni mke mdogo.
Miongoni mwa wanafamilia wa marehemu Komba.
Mwili wa marehemu John Komba ukiingia Karimjee ili kuagwa na wananchi na viongozi leo jijini Dar.
No comments:
Post a Comment