Mimi nimezaliwa na kukulia uswazi wakati waifu wangu ni wa kishua. Jamii niliyokulia (hukoo uswazi kwetu) kuna katabia ka kuwapa watoto majina kulingana na matukio maarufu yanayotokea au majina ya watu maarufu. Mfano kuna watoto wanaitwa cossovo, sunami, osama, michael jackson (kipindi alivokufa), obama, samunge, neymar, baloteli nk....
Kasheshe inakuja kwamba mke wangu amejifungua kidume sasa mimi nimependekeza tumwite "UKAWA" (kwasababu ndio jina lililobamba kwa sasa Tz) lakini wife haelewi wala hasikii.
Ubaya au uzuri jina hili limekubalika sana kwa ndugu na marafiki zangu. Sasa wadau hapo ndipo ninapovurugwa maana mwenyewe nilikua naomba sana mwanetu azaliwe kukiwa na tukio kubwa ili na mimi niadopt vizuri utamaduni wetu.
Credit: udakuspecially
No comments:
Post a Comment