February 14, 2015

SHTUKA! KWA NINI MKE WA MTU ANAKUWA MKE WA WATU-2





HATUNA budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutukutanisha tena katika uwanja wetu maridhawa wa kupeana darasa la uhusiano. Siku zote ukikubali kupokea na kufanyia kazi yale tunayopeana kila Jumamosi kupitia safu hii.

Leo ni siku ya wapendanao (valentine‘s day). Ni vyema basi ukaitumia siku hii kutafakari na umpendaye. Kumpa zawadi, kutafuta sehemu tulivu na kujadili uhusiano wenu.Ifanye siku hii kuwa mwanga mzuri wa penzi lenu. Kama mligombana, tumieni nafasi hii kuombana msamaha na kuanza upya safari yenu. Usikubali kuendelea kuishi katika penzi ambalo halina mwanga wa mbeleni. 

Kwa siku hii ya leo, si lazima uoneshe upendo kwa mpenzi wako pekee, unaweza pia kuonesha upendo kwa baba, mama, rafiki na watu wanaokuzunguka. Watakie sherehe njema ya valentine. 

Kwa wale tuliokuwa pamoja wiki iliyopita, tulikuwa na mada yetu iliyohusu mke wa mtu kuwa mke wa watu. Nilieleza namna ambavyo mke wa mtu anavyoweza kuangukia katika dmbwi la kuwa mke wa watu kwa sababu ya kukosa umakini. 

Anashindwa kujua kwamba kama mke wa mtu anapaswa aishi vipi na ndugu, jamaa na marafiki ili asitoe mwanya wa watu kumfanya mke wa watu.Tumalizie mada hii kwa kutazama mazingira na vichocheo vinavyowasababisha mke wa mtu ageuke kuwa mke wa watu. Mbali na kujua vichocheo hivyo, pia tutapata kujua mbinu mbalimbali za kuepukana na tatizo hili: 

UMBALI
Unapokuwa umeolewa moja kwa moja utakutana na mashemeji utakutana na marafiki wa kiume kama vile ulivyokuwa hujaolewa. Suala la msingi hapa ni mabadiliko. Unatakiwa kubadilika ili usiweze kutoa mwanya wa vishawishi. 

No comments:

Post a Comment