February 14, 2015

AIBU NZITO: MSANII MWENYE HESHIMA TZ, STARA THOMAS AFUMANIWA LIVE!

Staa wa Bongo Fleva, Stara Thomas akiwa na mumewe.
Stori: Deogratius Mongela na Chande Abdallah/Risasi 
HAYA ni madai mazito! Kwamba, staa wa Bongo Fleva ambaye juzi kati alinusa kwenye gospo ‘ikamshinda', Stara Thomas anadaiwa kufumaniwa na mumewe, Raumu Ally mpaka kufikishana polisi, Risasi Jumamosi halipitwagi na ‘ubuyu’. 

Kwa mujibu wa shuhuda wa kuaminika, tukio hili lilijiri hivi karibuni nyumbani kwa familia hiyo, Tabata jijini Dar es Salaam. 

FUMANIZI LILIVYOTOKEA
Akilisimulia Risasi Jumamosi baada ya kuulizwa kama kweli fumanizi lilikuwepo, mume wa Stara alifunguka hivi: “Ni kweli ilitokea. Siku ya fumanizi nilikuwa nimesafiri, lakini nikarudi ghafla bila kumpa taarifa mke wangu.
 “Nilikuwa nyumbani, yeye hakuwepo. Saa 9:00 usiku ndiyo nilimwona Stara akirejea tena akiwa amelewa. Aliletwa na gari mpaka nje ya nyumba.” 

NDANI YA GARI KWA NUSU SAA
“Lile gari lilisimama zaidi ya nusu nje bila kushuka mtu ndipo nikaamua kulifuata. Stara aliponiona akamwambia dereva ambaye najua ni jamaa yake, aondoe gari kwani mimi ni mume wake nitampiga.

“Nilizuia wasitoke, yule jamaa akarudi nyuma na kuniparuza kwenye mguu na tairi, nikadondoka. Niliposimama nikaokota jiwe na kulirushia gari nikavunja kioo cha mbele.” 

STARA, JAMAA POLISI
Mume huyo anaendelea kusimulia: “Baada ya hapo Stara aliondoka na yule jamaa mpaka Kituo cha Polisi Tabata ambapo walinishtaki. Niliitwa polisi kwa madai ya uharibifu wa kioo.

“Kwa vile nilikuwa nasafiri kwenda nje ya nchi (ni dereva wa malori) niliona mambo yaishie pale kituoni, nilikwenda nikachukuliwa maelezo kisha nikalipa shilingi laki saba (700,000).”

Mume wa Stara Thomas Raumu Ally.
 DALILI ZA KUVUNJIKA KWA HESHIMA
Habari zaidi zilidai kwamba, wawili hao wamekuwa kwenye ugomvi wa mara kwa mara.


Imeelezwa kwamba, ugomvi wao ulianza pale Raumu aliposhindwa kulipa ada ya shilingi laki tano ya mtoto wa Stara (jina tunalo) huku madai ya mchepuko nayo yakisambaa hali iliyokuwa ikishusha heshima ya familia. 

TUJIUNGE NA RAUMU 
Akifafanua kuwepo kwa sakata hilo pamoja na chanzo kizima, Raumu alisema kuwa Stara amekuwa akimfanyia vituko na mambo ya ajabu tangu aliposimamishwa kazi kwenye kampuni aliyokuwa akifanyia awali (jina kapuni) baada ya kutokea matatizo. 

No comments:

Post a Comment