January 28, 2015

Wema Sepetu: Huyu ndio “my Idol” kwenye kuigiza!!


Anaitwa Taraji Penda Herson, aliezaliwa miaka 44 iliyopita huko Washington, USA. ni moja kati ya waigizaji wakubwa wa huko Hollywood, ni mama wa mtoto mmoja na anaishi kama “Single Mother” ameshasheza tamthilia, vipindi vya televisheni na filamu mbalimbali zikiwemo  Think Like a Man,Madly Madagascar ,Think Like a Man Too na No Good Deed alizozicheza miaka ya hivi karibuni.
Chakushangaza sasa majina yake  mawili ya kwanza yana asili ya kiswahili kabisa  “Taraji"  na  "Penda"  wanayatafsiri kama “hope” na “love” kwa lugha ya kingereza. labda  inawezekana akawa ana asili ya huku afrika ya mashariki
Sasa hivi anaendesha kipindi cha televisheni kinachoitwa Empire kinachirushwa na "channel" ya FOX.
Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram mwigizaji Wema Sepetu alitupia picha za taraji na kuandika kuwa linapokuja swala la kuigiza yeye anampenda na angependa kuwa kama yeye. Haya ndio maneno ya Wema;
“This Woman Tho..... Talk abt my idol wen it comes to acting.... Ladies and Gentlema.....Taraji..Cookie Isnt she just something.... I jus love her”-Wema alimaliza

No comments:

Post a Comment