Mwanamume mmoja aitwaye John Haule(35) mkazi wa kijiji cha Lupapila,manispaa ya Songea amefariki dunia ghafla wakati akifanya mapenzi na mpenzi wake Winfrida Ndalama(35) nyumbani kwa huyo mpenzi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana,kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema tukio hilo limetokea Januari 17 mwaka huu saa 8 usiku katika kijiji ch Subira manispaa ya Songea.
"Siku ya tukio Haule alienda nyumbani kwa mpenzi wake saa 2 usiku akitokea hospitali ya Misheni ya Peramiho ambako akikwenda kumuuguza mjomba wake"
"Alipokuwa hospitalini,alimuaga mjomba wake kuwa amemkumbuka mtoto wake mdogo mwenye umri wa miezi 11,hivyo anatamani akamwone na angerudi hospitali.
"Mjomba wake alimruhusu aondoke lakini kwa bahati mbaya Haule hakufika nyumbani kwake na badala yake alipitiliza hadi nyumbani kwa mpenzi wake(nyumba ndogo)",alieleza kamanda Msikhela.
Kamanda huyo alisema wakati Haule akiwa nyumbani hapo,Winfrida alimwandalia chakula,lakini alikataa kula kwa madai kuwa alikuwa ameshiba.
"Lakini ilipofika saa tatu usiku walikwenda kulala na kufanya tendo la ndoa kisha wakapumzika,Ilipofika saa nane usiku,Haule alimwomba mpenzi wake huyo wafanye tena tendo la ndoa,lakini alikataa kwa madai kuwa amechoka,lakini baada ya kumlazimisha alikubali,wakaanza kufanya lakini walipokuwa wakifanya ghafla mwanamume huyo alianza kukoroma huku akitetemeka kisha kufariki dunia".
"Baadaye taarifa zilipelekwa katika ofisi ya serikali ya mtaa kisha zikafikishwa polisi ambako mwanamke huyo alikamatwa na anashikiliwa kwa mahojiano zaidi",alisema kamanda huyo.
Na Amon Mtega-Songea
No comments:
Post a Comment