January 27, 2015

MWANAMKE AWAUA WATOTO WAKE WAWILI NA KUWAZIKA NDANI YA NYUMBA YAKE TABORA


Mwanamke mmoja  mkazi wa mkoa wa Tabora wilaya ya Tabora mjini kata ya Chemchem amewaua watoto wake wawili  na kuwazika ndani ya nyumba yake.Mwanamke  huyo  amedai  kuwa  kilichomfanya  awalishe  sumu  watoto  wake  ni ugumu  wa  maisha  uliokuwa  ukimkabili  baada  ya  kikimbiwa  na  mumewe. 
Kwa  mujibu  wa  jirani  yake, siku  ya  tukio  mwanamke  huyo  alisikika  akichimba  shimbo  ndani  ya  nyumba  yake  kabla  ya  kutangaza  kupotelewa  na  watoto  wake  siku  ya  pili  yake.

Taarifa  ya  kupotea  kwa  watoto  hao   ilimpa  mashaka  jirani  huyo  na  kumlazimu  akatoe  taarifa  polisi  ambapo  maafande  walikuja  na  kufanya  msako  ndani  ya  nyumba  hiyo  ambapo  walifanikiwa  kufukua  maiti  za  watoto  hao.

No comments:

Post a Comment