Tukio hilo lilitokea juzikati kwenye gereza lililopo Mji wa Macau ambapo Wema aliambatana na meneja wake, Martin Kadinda pamoja na shemeji yake, Petit Man.
Chanzo kilicho karibu na Wema kimeeleza kuwa, Wema alipofika na kuona mazingira ya upweke ambayo Jack anaishi, aliwaza kwa muda na kuzungumza maneno kama mtu aliyechanganyikiwa hivyo kuwatia hofu Martin na Petit.
“Ilikuwa mshikemshike, alimmis sana Jack sasa alipomuona na mazingira yale ya upweke ndicho kilichomchanganya Wema lakini baadaye kina Martin walimrudisha kimawazo na hatimaye akawa sawa,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:“Hata hivyo, Wema amesema mazingira ya kule ndani siyo mabaya lakini kilichomuumiza yeye ni upweke ambao anao na watu wanaomzunguka.”
Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China.
Agosti, mwaka huu Jack Patrick ilielezwa kuwa alihukumiwa kifungo cha miaka sita jela huku kukiwa na uwezekano wa kupunguziwa adhabu endapo ataonesha utiifu gerezani.
No comments:
Post a Comment