October 24, 2014

MAJAMBAZI YAPORA BENK MAMILION ....YAONDOKA NA STAILI MPYA NA YAAJABU CHEKI HAPA..


Benki ya Stanbic tawi la Mayfair, Msasani, Dar, leo imevamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi na kupora kiasi kikubwa cha pesa.
Wamekuja na Noah nyeusi wakapark kama wateja. Walikua wawili, mmoja akapanga msitari mwingine akaenda kujaza fomu za kuchukulia hela. Yule alopanga msitari akafunga mlango na yule Askari akakunjwa akanyang'anywa alarm. Yule alokuwa anajaza fomu kawambia wateja nyote lala chini, alikua anamjua mwenye ufunguo, wakasema Anna leta huo ufunguo. Akataka kugoma walipomnyoshea mtutu akatoa. wakaingia Kwenye chumba cha hela wakakomba hela zote wakapakia kwenye Noah.
Wakawaaga na kusema iteni hao Polisi wenu. Hamna aliyeumizwa zaidi ya Askari kukunjwakunjwa alipotaka kubonyeza alarm.

chanzo;jamii forum

No comments:

Post a Comment