October 27, 2014

VIKAO VYA HARUSI VYA STAA WA MZUIKI BONGO VYAINGIA DOSARI...NI BAADA YA MSIBA KUTOKEA

Vikao vya maandalizi ya harusi ya msanii wa muziki Bongo, Isabela Mpanda vimeahirishwa na kusogezwa mbele baada ya kupata msiba wa dada yake. 
Msanii wa muziki Bongo, Isabela Mpanda.
Akizungumza na gazeti hili, Isabela alisema vikao vya maandalizi vilikuwa vianze Jumapili iliyopita lakini waliahirisha kutokana na msiba hivyo familia imeamua wasubiri mpaka siku arobaini ziishe ndipo waendelee na maandalizi ya harusi. 

“Dada yangu Fau ameniuma sana jamani hivyo kikao changu cha kwanza cha maandalizi ya harusi kimepelekwa mbele mpaka arobaini iishe ndipo mambo hayo yaendelee,”alisema Isabela.
Isabela na mpenzi wake wa siku nyingi, Luteni Karama wanatarajia kufunga ndoa mwishoni mwa mwaka huu ambapo Isabela amekuwa akifanya maandalizi ya nguo kabla hata vikao vya maandalizi kuanza.

No comments:

Post a Comment