October 27, 2014

KABANG!!ULISHAWAHI KUMUONA ROSE NDAUKA WA BONGO MOVIE AKIKATA MAUNO LEO TAZAMA HAPA


Baada ya kuachana na aliyekuwa mchumba’ke, Malick Bandawe kisha kurudi kwao, Kigogo jijini Dar, staa grade one wa Bongo Movies, Rose Donatus Ndauka anadaiwa hivi sasa hakamatiki hivyo hakauki viwanja. 
Staa grade one wa Bongo Movies, Rose Donatus Ndauka akiinjoi uhuru wa kuwa 'Single' Viwanja.
Uchunguzi wa Ijumaa Wikienda ambalo limekuwa likimnyatia kwa ukaribu Rose unaonesha kwamba tangu ametengana na mwanaume huyo amekuwa huru kupita maelezo huku akionesha jeuri ya fedha kama ilivyokuwa kwa mastaa wenzake, Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja.
Rose Ndauka akianza kukata mauno.
Pia uchunguzi huo ulibaini kwamba, mara tu baada ya kutoka ‘kifungoni’, Rose aliangusha bonge la sherehe ya ‘bethidei’ yake ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Collosseum, iliyopo Kariakoo jijini Dar na ndiko alikoanza kuonesha jeuri ya fedha.
Rose Ndauka akimwagia midolari mtangazaji wa Times FM, 'Dida'.
Data zilionesha kwamba siku tishio ni ile ya Oktoba 18, mwaka huu ambapo Rose alikuwa kinara wa ushangiliaji wa timu yake ya Yanga, jambo ambalo siku za nyuma alikuwa hafanyi hivyo.
Siku hiyohiyo, baada ya kutoka uwanjani alikwenda kubadilisha mavazi yake ya njano na kijani kisha akatupia pamba za kuruka viwanja, akaibuka katika Tamasha la Fiesta kwenye Viwanja vya Leader, Kinondoni jijini Dar.
Rose Ndauka akiendeleza mauno.
Akiwa ndani ya Leaders, Rose aliambatana na Mtangazaji wa Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ ambapo alikuwa akihaha kumnasa mwanamuziki wa Marekani, T.I aliyetimba Bongo kutumbuiza kwenye tamasha hilo.

Kama hiyo haitoshi, Alhamisi iliyopita, Rose alithibitisha kwamba kwa sasa hashikiki kwani alitimba kwenye pati ya bethidei ya shoga’ke, Dida iliyofanyika nyumbani kwake, Mwananyamala, Dar ambapo alikuwa kinara wa kujiachia kwa kusakata muziki na kumwaga ‘madolari’.
Wasanii wa Bongo Movies 'Riyama' na 'JB' wakiwa na Rose ndauka katika Viwanja hivyo.
Ulipofika muda wa muziki, hapo ndipo Rose alipopagawa na kujikuta akikata mauno huku akipiga kelele ‘raha jipe mwenyeweee…’
Mwanahabari wetu alipotaka kujua kulikoni Rose kujiachia kiasi hicho, aliomba aachwe afurahie maisha.

No comments:

Post a Comment