Mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Mwanaheri anadaiwa kunaswa kwa msala wa utapeli na kupewa kashikashi la aina yake baada ya ‘kutaitiwa’ na wanawake wenzake ambao ni wajasiriamali akisemekana kukomba mali zenye gharama za Sh. milioni mbili.
Mtuhumiwa (Mwanaheri) aliyenaswa kwa msala wa utapeli akiwa chini ya ulinzi wa Polisi eneo la Mlimani City jijini Dar.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na wanahabari wetu lilijiri Mlimani City jijini Dar, mapema wiki hii, mishale ya saa 10:00 jioni ambapo Mwanaheri aliwekewa mtego na wanawake hao wanaofanyia bishara zao Kariakoo.
Kwa mujibu wa wanawake hao, Mwanaheri alikuwa akiwasumbua kwa muda mrefu bila kurejesha pesa za mali walizompatia katika kikundi chao ambacho kinajishughulisha na kuuza bidhaa za Forever Living.
“Mwanaheri aliingizwa kwenye kikundi na mama yake mdogo (jina kapuni), tukamwamini na kumpatia mzigo wa Sh. milioni mbili.Kikosi kilichomnasa tapeli Mwanaheri kikiwa kazini.
“Cha kushangaza Mwanaheri aliondoka na hakuonekana tena, kila tukimpigia simu hapokei na mama yake mdogo akimpigia anamtukana ndiyo maana tukampangia mpango wa kumkamata ambao umekamilika leo,” alisema mmoja wa wanawake hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Zainabu. “Mwanaheri aliingizwa kwenye kikundi na mama yake mdogo (jina kapuni), tukamwamini na kumpatia mzigo wa Sh. milioni mbili.Kikosi kilichomnasa tapeli Mwanaheri kikiwa kazini.
Mama huyo alidai kuwa baada ya kuona wamekosa njia ya kumkamata waliamua kumtafuta mtu aliyejifanya kuwa ni mteja na kumpa namba yake ambaye aliomba wakutane Mlimani City kwani alikuwa akihitaji mzigo mkubwa.Umati wa watu wawaliokuwa eneo la tukio wakimshuhudia tapeli huyo.
“Bila aibu sijui alikwenda kutapeli kwa nani tena akakubaliana na mteja wakutane Mlimani City ndiyo tukajipanga na kuja kumkamata.
“Alipopigiwa na mama aliyeahidiana naye akaja na mzigo lakini alipotuona akaanza kukimbia tena alikuwa na wenzake, tuliamua kumkimbiza na kumtia nguvuni,” alisema Zainabu.
Hadi gazeti hili linaondoka eneo la tukio, wanawake hao wakishirikiana na walinzi wa Mlimani City walimwingiza Mwanaheri kwenye gari na kumpeleka kumuhoji kisha kumpeleka polisi ili kumfungulia kesi ya madai.
No comments:
Post a Comment