TUMUOMBEE! Hali ya kiafya ya staa mkubwa wa Injili Bongo, Rose Muhando siyo nzuri na amewaomba Watanzania wamuombee kwani ni mgonjwa...
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum katikati ya wiki hii, Rose ambaye ameripotiwa kwa misala tofauti ya kuchikichia fedha za shoo hivi karibuni, amefunguka kuwa afya yake si nzuri kwani anasumbuliwa na mshipa kwenye mguu, akafanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Mkoa ya Dodoma.
“Siko vizuri kiafya nimefanyiwa upasuaji mguuni, nimeshonywa nyuzi nne lakini bado hali yangu si nzuri kiafya, nawaomba Watanzania waniombee,” alisema Rose kwa tabu na kuongeza:
“Hata ukiniona utanihurumia kwani mbali na upasuaji kwenye kidole gumba pia nimevimba sana uso.
“Kwa sasa nipo kitandani nyumbani kwangu najiuguza. Nitarudi tena hospitalini Jumanne ijayo.”
Akizidi kumwaga maneno kwa kinasa sauti cha Risasi Jumamosi, Rose alimshukuru mwandishi wa Barua Nzito iliyochapishwa katika gazeti tumbo moja na hili la Risasi Mchanganyiko (toleo lililopita) kwa kumuonya juu ya suala la kudaiwa kuingia mitini na fedha tofauti za shoo na kuomba radhi kwa Watanzania.
“Nawaomba sana radhi wote niliowakosea, niwaombe waniombee nipone na nitarejesha fedha zao,” alisema Rose.
Tunamuombea Rose kwa Mwenyezi Mungu ampe afya njema ili aendelee na huduma ya kumtumikia Mungu kwa njia ya nyimbo za Injili-Mhariri........@
October 25, 2014
ROSE MHANDO AFANYIWA UPASUAJI....MAOMBI YAKO NI UHIMU KWAKE SOMA ZAIDI HAPA....
Tags
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment