
Kwa mujibu wa chanzo makini, tukio hilo lilitokea saa 6 mchana wakati wazazi wa mtoto huyo wakiwa kazini na kuacha ufunguo kwa mmiliki wa nyumba aliyejulikana kwa jina la mama Fau.Chanzo hicho kilieleza kuwa siku ya tukio, Focus alirejea nyumbani kutoka shuleni na kumuacha mdogo wake, Irene Steve (5).
Akizungumzia tukio hilo, mtoto Irene alisema baada ya kumkuta Fucus akining’ing’inia hakuamini mara moja kama amefariki dunia.

Akizungumza na mwandishi wetu, mama mdogo wa Irene, Catherine Zakaria alisema naye hakuamini tukio hilo.“Aliponiambia Focus kaning’inia mlangoni nilishtuka, nikakakimbilia eneo la tukio na kukuta kweli.“Ila mimi naamini kuna mtu alimnyonga kwa kutumia gauni la ndugu yake, nasema wamemnyonga kwa sababu mazingira ya tukio asingeweza kujitundika juu ya komeo mwenyewe kwa umri wake na kimo chake,’’ alisema Catherine.

Akizidi kufafanua juu ya mazingira aliyoyakuta, Catherine alisema alishangaa wakati akihangaika kuita majirani, aliporudi aliukuta mwili umeshushwa chini.
“Niliukuta mwili wa marehemu ukiwa umening’inia juu ya mlango lakini katika kutoka kuita majirani, kurudi nikakuta mwili umeshushwa chini, nilipojaribu kuuliza ni nani aliyeushusha, hakuna aliyenijibu,’’ alisema Catherine.Akizungumzia tukio hilo, mmiliki wa nyumba hiyo, mama Fau, alisema alishtushwa na tukio hilo.
Mama wa marehemu, Rehema alisema anaumia kukuta mwanaye amefariki dunia na kuomba vyombo vya dola vifanye kazi yake kikamilifu.
No comments:
Post a Comment