
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya, Dk. Adam Sijaona, amethibitisha kupokea miili ya watu hao, Mwanafunzi wa darasa la nne Shule ya Msingi Ukombozi Reginald Robert (9), Sophia Robert (6) (darasa la kwanza)na Remijius Robert (4).
Dk. Sijaona aliwataja waliojeruhiwa sehemu za kifua, kichwani, mikono na miguu na makalio kuwa ni baba wa familia hiyo, Robert Remijius (45), mkewe, Angelina Gaspar (42) na mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Mwatulole, Scolastica Robert (15), aliyehamishiwa hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza kutokana na kuungua vibaya.
No comments:
Post a Comment