September 18, 2014

EXCLUSSIVE!!MAANDAMANO YA CHADEMA YAANZA DODOMA...HALI NI TETE CHEK

Mnamo september 14 mwaka huu mh:freeman mbowe wa chadeama alitangaza kuhitisha maandamano ya nchi nzima kupinga uwepo wa bunge la katiba linaloendelea hivi sasa hapa mjini dodoma kwa madai ya mchakato huo kutumia fedha za wananchi pasipo manufaa yoyote ya msingi.


Katika mkoa huu wa dodoma maandamano hayo yanaanza leo hii katika maeneo mbali mbali ikiwapo eneo la bunge ambapo kwa kiasi kikubwa ndio chanzo cha maandamano haya. Kwa muda huu jeshi la polisi limeweka ulinzi mkali ambaoumelenga kuimarisha amani mkoani hapa.

Katika maeneo ya mikusanyiko ya watu hasa eneo maarufu sana mkoani hapa la nyerere squre wapo polisi wenye farasi na pia waenda kwa miguu wakizunguka maeneo hayo wakiangalia nini kitatokea mnamo mida ya saa tano ambapo ndipo mwenyekiti wa chadema mkoani hapa bwana Jela Mambo alitangaza rasmi kuanza kwa maandamano wakianzia bungeni.

Licha ya polisi kuwepo nyerere squre pia wameweka uzio katika eneo la bunge kuwazuia waandamanaji hao kufika hapo na kuleta msongamano usiokuwa na tija kwa raia wengine,lakini pia kutokea hapo, kumewekwa uzio hadi ilipo stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na kusababisha hadha kubwa kwa magari yaendayo mikoa ya morogoro na dar es salaam..





Hata hivyo kaimu kamanda mkuu wa mkoa wa dodoma bwana Emmanuel Lukula  alitangaza kuwa maandamano hayo hayana kibali kutokana na sheria ya kuwasilisha taarifa ndani ya masaa 48 kabla ya kufanyika maandamano husika jambo ambalo Chadema walikiuka kwa kuwasilisha barua yao hapo jana mida ya saa tano kwa baadhi ya maeneo hivyo alitangaza kutoyatambua maandamano hayo na kuwataka wananchi kutojihusisha na maandamano hayo kwani kisheria hayajaruhusiwa.

Hivi karibuni mwenyekiti wa Chadema freeman mbowe alitangaza kuandamana huku akiwataka wanachama kuwa tayari kwa maandamano hata ikiwezekana kumwaga damu kwa ajili ya kutetea nchi yao kutokana na kile alichoda kuwa ni serikali kutumia vibaya mali ya umma.
credit omwatani blog....#

No comments:

Post a Comment