Mapenzi ni kitu kilichotawala dunia kwa sasa kwani hata unapoanza kujuana na mtu yeyote yule kati ya maswali matano atakayo kuuliza lipo lile la je unamchumba sasa fahamu hapa baadhi ya sentensi ambazo ukizisikia kutoka kwa mpenzi wako jua anakudanganya kwa mjibu wa utafiti uliofanyika
1.Ungejua wala sina haraka ya kuolewa!
Hakuna mwanamke ambaye yuko tayari kuona umri unamkimbia, ameshahudhuria
harusi za marafiki zake, pengine ameshaliona mpaka gauni
litakalompendeza harusini halafu eti akuambie hana haraka ya kuolewa!
2. Ngoja Nikavae, nipe dakika tano tu!
Ukiambiwa hivi, basi Kama hujanywa soda muda mrefu huu ndo muda muafaka!
Tafuta sehemu yenye utulivu upate kinywaji chako maana hizo dakika tano
ni dakika hamsini!
3.Wala sioni wivu ukiwa unawaangalia wanawake wengine
Akikuambia hivi, anataka tu akuonyeshe ni jinsi gani amekua kiakili, na
ni mtu muelewa saana.. lakini moyoni mwake anatamani kukupiga makofi
unapomuangalia msichana mwingine huku akijiuliza moyoni, kwani huyo
anaemuangalia amenishinda nini?
4.Hata kama unapata mshahala mdogo, mi nimeridhika kabisaa.. (mmmh Kweli?)
5.Mbona dada yako hajaja kututembelea muda mrefu? sana!
Mara chache sana kutakuwepo na upendo kati ya mpenzi wako na dada yako
au hata mama. Kwa mwanamke ni bora umletee wadogo zako wa kiume kumi
nyumbani atawalea ila sio dada yako mmoja!
6.Napenda Kila kitu kutoka kwako
Unadanganywa! lazima kuna kitu angalau kimoja angependa ubadilike au
anapanga kukubadilisha.. mara nyingine atataka hata uwe kama Yule kaka
anayemuona kwenye tamthilia!
7.Sihitaji Kuwa na mwanaume kwa sasa.
Niko â€Å“busy†sana! Au utaambiwa nimeumizwa sana hata kama yeye ndiye
mgonvi namba moja!
8.Wala sina njaa, mi nikila kidogo tu nashiba!
9. Niko sawa tu, hamna shida!
Ukweli ni kwamba anataka uongeze juhudi kumbembeleza ili akuambie ni
nini shida.

No comments:
Post a Comment