Waziri mkuu Mizengo Pinda.
HALI si shwari mitaani inapotokea habari ya kuzungumzwa inahusu Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kufuatia ajenda yao ya kujiengua kwenye Kikao cha Bunge Maalum la Katiba linaloendelea kwa sasa mjini Dodoma.Hali hiyo imekuja kufuatia Agosti 4, mwaka huu, wakazi wawili wa jijini Dar kutwangana ndani ya baa moja (jina lipo) iliyopo Tabata Kisukuru, Dar kisa kikiwa kila mmoja kuegemea makundi ya kisiasa.
Wakazi hao walikuwa wamekaa kwenye meza mbili tofauti lakini kila mmoja alikuwa na wenzake wengine. Ndipo jamaa mmoja kwenye meza yake alianzisha mazungumzo yenye dalili zote za kuwalaumu Ukawa kwa kujitoa bungeni.
Maneno ya jamaa huyo hayakuvumiliwa na yule aliyekaa kwenye meza nyingine ambapo alimjia juu huku akidai ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kumwambia Ukawa wana hoja bali CCM ndiyo wa kulaumiwa.
Samuel Sitta.
Wawili hao walitupiana maneno makali mpaka wakafikia hatua ya kushikana mashati na kutwangana, hali iliyozua tafrani kwenye baa hiyo, hususan kwa wateja ambao hawakuwa na kundi lolote.Kwa sasa sehemu kubwa ya mazungumzo ya watu mitaani, hasa kwenye miji mikubwa ni kuhusu Ukawa kujitoa bungeni huku wajumbe wengine wasiowaunga mkono wakishiriki kikao cha bunge.
Hali hiyo imekuwa ikisababisha baadhi ya watu kutofautiana waziwazi hadi pale watakapoamua kuachana na habari ya Ukawa.
No comments:
Post a Comment