Imefichuka!
Baada ya kuitwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa ajili ya kupongezwa
kutokana na tuzo aliyopata nchini Nigeria, staa wa filamu, Elizabeth
Michael ‘Lulu’ alijikuta akihaha baada ya kuzuiwa kuingia Ikulu kutokana
na kutokuwa na kitambulisho cha chama cha waigizaji.
Chanzo
makini kililiambia gazeti hili kwamba Lulu alijikuta katika wakati
mgumu kwani utaratibu wa wasanii kuingia Ikulu umebadilika, tofauti na
serikali iliyopita kwani kwa sasa, wasanii wa filamu ni lazima wapitie
kwenye Shirikisho la Filamu ‘TAFF’ kisha wizarani ndipo waruhusiwe
kuonana na mhusika aliyemuita au anayetaka kumuona.
“Shughuli
ilikuwa ifanyike Alhamis, Lulu alipofika wizarani akakutana na
utaratibu huo mpya, si unajua yeye siyo mwanachama wa chama chochote cha
filamu, ndiyo ikabidi aelezwe jambo hilo,” kilisema chanzo hicho.
JFKutokana
na utaratibu huo, Lulu akalazimika kurudi katika ofisi za mwenyekiti wa
waigizaji mkoa wa Kinondoni (TDFAA), Ally Baucha ambapo alichukua fomu
ya uanachama na kuijaza na kuirejesha siku hiyohiyo ya Alhamis
iliyopita ili aweze kwenda kuonana na Waziri Mkuu siku iliyofuata
(Ijumaa). “Yaani Lulu alihangaika kweli siku hiyo kwani hata siku ya
kupokelewa pale Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere hakuna msanii wa TAFF
aliyekwenda kumpokea hata mmoja wala viongozi wake, hivyo hata
alipopata mwaliko wa Ikulu ikashindikana kuingia bila ya utambulisho wa
uanachama wa shirikisho na chama cha waigizaji mkoa anaoishi wa
Kinondoni,” kilisema chanzo hicho.
Baada
ya kuzinyaka habari hizo paparazi wetu alimtafuta Mwenyekiti wa TDFAA,
Ally Baucha ambapo alikiri kwamba ni kweli Lulu alikwenda kuchukua fomu
harakaharaka na kuijaza na kuwa mwanachama ikiwa ni baada ya kupata
mwaliko wa kwenda kupewa pongezi na Waziri Mkuu.
Naye
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba ni kweli kwa sasa hakuna
msanii anayeruhusiwa kuingia Ikulu bila kupitia kwenye shirikisho na
wizarani hata kama ameitwa na nani.
“Utaratibu
umebadilika sasa, msanii hata kama ameitwa na kiongozi gani ni lazima
afuate utaratibu huo ndivyo tulivyokubaliana, hivyo Lulu alishindwa
kwenda moja kwa moja mpaka alipokwenda kujiunga kwanza na chama cha
waigizaji na kutambulika na shirikisho ndipo nikawapeleka Ijumaa
iliyopita na msanii mwenzake aliyeshinda tuzo pia, Single Mtambalike
‘Richie’ na kwenda kupongezwa kwa kutwaa tuzo hizo za kimataifa.
“Wasanii
wanatakiwa kuufahamu utaratibu huo kwani hata wakipita moja kwa moja
lazima watarudishwa tu kwenye shirikisho, wakati wao ukifika kama Lulu
naamini watajiunga tu hatumlazimishi mtu,”alisema Mwakifwamba.
Hivi
karibuni, wasanii hao wawili walishinda Tuzo za African Movies Viewers
Choice (AMVC) zilizofanyika nchini Nigeria ambapo Lulu alishinda katika
Kipengele cha Filamu Bora ya Afrika Mashariki (Mapenzi ya Mungu) huku
Richie akichukua kwenye Kipengele cha Filamu Bora ya Kiswahili Afrika
Mashariki (Kitendawili), tukio lililofanyika Nigeria wiki iliyopita.
Chanzo:Global Publishers
March 18, 2016
Home
/
Unlabelled
/
Mwigizaji Lulu Azuiwa Kuingia Ikulu Kuonana na Waziri Mkuu...Kisa Kizima Kipo Hapa...
Mwigizaji Lulu Azuiwa Kuingia Ikulu Kuonana na Waziri Mkuu...Kisa Kizima Kipo Hapa...
Tags
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment