Mage Sibonike akiwa na maumivu makali baada ya kupewa kichapo na wifi yake.
Katika tukio hilo la kutisha lilijiri hivi karibuni maeneo ya Soweto
mkoani Mbeya ilidaiwa kwamba, Ester alikuwa akimshuku mumewe kuwa ana
mchepuko.Chanzo chetu kilidai kwamba, katika maisha yao, Ester na mumewe
wamejaliwa mtoto mmoja.
Ilisemekana kwamba, siku ya tukio, Ester alimfuatilia mumewe ambapo
aligundua kuwa anakwenda kuonana na mwanamke aliyetajwa kwa jina Fetty
Mchina, karibu na nyumbani kwa mama mkwe wake.
Ester Mjila anayedaiwa kumjeruhi wifi yake.
Ilidaiwa kuwa, baada ya Ester kutega kwa muda mrefu maeneo hayo,
alimuona mzazi mwenziye huyo akiwa kwenye grosari ya dada yake
aliyetajwa kwa jina moja la Mage, wakiwa kimalavidavi na Fetty Mchina
huku pembeni yao akiwemo wifi yake huyo.
Ilielezwa kwamba, uvumilivu ulimshinda ndipo akaanzisha timbwili ‘hevi’
bila kuuliza ambapo katika varangati hilo huku chupa zikirushwa, mumewe
na Fetty Mchina walitoka nduki na kumuachia msala wifi mtu.
Ilidadavuliwa kwamba, katika hali ya kushangaza umati uliofurika na
kufunga mtaa, baada ya kutandikana makonde, Ester alivunja chupa tupu ya
bia ambayo aliitumia kumchanachana wifi yake huyo na kumsababishia
majeraha makubwa mwilini.
Moja ya jeraha mguuni.
Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kuwa, mama mkwe aliyekuwa nje
nyumbani kwake alisikia mayowe na kufika eneo la tukio ndipo Ester
akamuhamishia kipigo mama mkwe wake kwa kumzaba makofi hadi akapoteza
fahamu.
Ilielezwa kwamba, baada ya Ester kuondoka eneo hilo, mumewe alifika na
kumchukua dada yake aliyekuwa hajiwezi na kumpeleka Hospitali ya Rufaa
ya Mbeya baada ya kupata PF-3 kisha Ester alikamatwa na kuwekwa ndani
katika Kituo cha Kati Mbeya Mjini kabla ya kuachiwa kwa dhamana.
Akizungumza kwa majonzi, mama mkwe huyo alisema kuwa alishangaa baada ya
kusikia mwanaye akipiga kelele na alipotoka aliona akipigwa na kuchanwa
na chupa na wifi yake.
Jeraha alilolipata usoni.
Alisema alipoingilia kati alipokea kipigo kutoka kwa Ester hadi akapoteza fahamu.
“Nilimkuta mwanangu anakwanguliwa kwa chupa, nilipojaribu kuamulia ndipo
nikapewa kipigo na mkwe wangu hadi nikazimia,” alisema mama huyo
aliyegoma kutaja jina lake.
Kaka mtu.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Mage ambaye bado anauguza majeraha
alisema kuwa alishtukia akivamiwa na mke wa kaka yake na kuchanwa kwa
chupa akituhumiwa kumuunganishia wanawake kaka yake, jambo ambalo siyo
kweli

No comments:
Post a Comment