December 4, 2014

MASHABIKI WA DIVA WA CLOUDS WATAKA KUANDAMA KUJUA ..DIVA YUPO WAPI MENEJA ATULIA KIMYA



Mashabiki wa kituo cha redio cha Clouds FM wiki hii wameungana na watu wengi mbalimbali kukipongeza kwa kutimiza miaka 15 tangu kianzishwe, lakini kuna kundi moja la watu halina furaha – mashabiki wa kipindi cha Ala za Roho kinachoendeshwa na Loveness aka Diva the Bawse. 

Kuna taarifa kuwa mtangazaji huyo mwenye mashabiki wengi, amesimamishwa kazi. Awali wasikilizaji wake waliambiwa kuwa Mrs GK, yupo likizo lakini baada ya kuona likizo ya mwezi mmoja inakuwa miezi, walianza kuhisi kuna kitu hakipo sawa.  

Kwa muda mrefu wamekuwa wakikitaka kituo hicho kuwapa majibu ya kwanini hawamsikii malkia wao bila kupata majibu. Wengine wamefikia hadi hatua ya kwenda kwenye kituo hicho kuuliza kunani na bado wanadai wahusika wamekuwa wakiwakwepa. 


Na sasa, mashambulizi yao wameyahamishia kwa meneja wa vipindi wa kituo hicho, Sebastian Maganga ambaye post yake ya juzi katika birthday ya Clouds FM iligeuka uwanja wao wa kumwaga malalamiko yao. 

“Brother @sebamaganga turudishiee #alazaroho na mrembo wetu @divathebawse tutaandamaanaa MZEE tujee mjengoniiii tumemis saut ya kumtoa nyoka pangonii please tunampenda @divathebawse yuko wapiii bnaaaah brother,” aliandika Young wa Leo. 

Mwingine aitwaye ‘mamaanithakeko’, aliandika:

Ninasikia wamemusimamisha kisa sijui alimuandika Zitto Kabwe twita huyo Zitto Kabwe na wasikilizaji wenu nani ana umuhimu na mnatudharau hamtujibu tukiwauLiza kipindi kinaboa au ndio mnataka tuhamie efm tukichagua nyimbo hampigi kila siku Daudi wa Kota. Leo nimekuja kuuliza diva yuko wapi mlinzi wenu kasema sisi wenyewe tunamtaka tumsikie usiku tumechoka likipindi siku hizi na tumeambiwa ntukuone wewe tunamtaka diva wetu hamtutendei haki rudisheni ala za roho ya Diva mamuziki pelekeni huko hatutaki mnatuchezea nyie.” 

“Dah!! bro @sebamaganga me siwezi kukaa na kitu rohoni wakati brother angu upo me ni mdau mkubwa saaana wa @cloudsfmtz afu ww ndo pm wetu tunaomba plz plz kama kuna tatizo limetokea ktk uongoz wenu ww na diva plz tunaomba muyamalize maana takliban mwez wa pil sasa unaenda ala za roho aiko hewan wengine sisi radio yetu ni moja tu tunayoiskiliza zaid ya clouds fm tu. Tunaomba mumrudishe diva kwenye kipindi chake tayr ala za roho kisha jijengea jina tena jina kubwa saaana..brother seba tunawapa wapizan wetu pakusemea cha msingi brother seba irudishe ala za roho ya diva tumekuwa atuna furaha kuona ala za roho.aiko hewan tumekuwa watu wa kulala mapema kwasababu diva ayuko hewan @cloudsfmtz ni radio ya watu watu wenyewe ndo sisi…sio sababubu pm kukaa kimya kama diva amekosea muiteni muyamalize ktk vipindi vya usiku akuna kama ala za roho tanzania na africa mashariki..diva, plz plz plz chonde chonde niko chin ya miguu yako pm seba tunaomba ala za roho ya diva irudi kama itawezeka juma 3 kirudi….nafikil PM umenielewa narudia tena nakuomba saaana ala za roho.irudi.kama zaman…naipenda saaaana @cloudsfmtz iko moyon nisengependa kuona kipindi kinagwaya wakati brother seba upo plz ala za roho muirudishe pamoja na diva mana kipindi ndo anakiwezea,” aliandika mwingine aitwaye B4Shizzle. 

Hata hivyo Seba hakuweza kuwajibu chochote mashabiki hao waliotaka kujua hatma ya Diva.

No comments:

Post a Comment