Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata
jumla ya watu 287 ambao ni dada poa pamoja na kaka poa katika operation
maalum iliyofanyika maneo mbalimbali ya Jiji hilo.
Operation hiyo ilitangazwa na kamishna wa kanda maalum mnamo Tarehe 7
mwezi wa 3 na kuazimia kuwakamata madada poa na makaka poa pamoja na
wateja wao ambao watakutwa wakiwanunua.
Katika mkoa wa kipolisi wa ilala operation hii imefanikiwa kuwakamata
jumla ya madada poa 51 kutoka katika maeneo mbalimbali yakiwemo
msimbazi,Buguruni,na stakishari,pia imewakamata jumla ya makaka poa 12
ambapo 11 wanatokea Buguruni na mmoja kutoka msimbazi.
Mkoa wa kipolisi wa temeke umefanikiwa kuwakamata jumla ya madada poa
22,ambapo changombe walipatikana 12,na mbagala walipatikana madada poa
10.
Aidha katika mkoa wa kipolisi wa kinondoni operation hiyo imefanikiwa
kuwakamata madada poa 76 kutoka maeneo ya osyterbay madada poa
49,magomeni 23,na kawe madada poa 4,pamoja na makaka poa 4.
Akizungumza na wanahabari jana makao makuu ya polisi kanda maalum ya Dar
es salaam ,Kamishna wa kanda hiyo CP Simon Sirro aliwataka watu wenye
tabia kama hizo kuacha mara moja kwani ni kinyume na mila na desturi za
mtanzania ambapo amewataka kutafuta biashara nyingine halali za kufanya.
March 15, 2016
Home
/
Unlabelled
/
MACHANGUDOA 287 Dar es Salaam Wakiona Cha Moto...Wakamatwa Pomoja na Wateja Wao na Kuswekwa Polisi
MACHANGUDOA 287 Dar es Salaam Wakiona Cha Moto...Wakamatwa Pomoja na Wateja Wao na Kuswekwa Polisi
Tags
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment