Ni ukweli kuwa Diamond na Alikiba ni wasanii ambao hawapatani kwa muda mrefu.
Kutokana
na ugomvi wao uliopo umepelekea mpaka mashabiki wao kuanzisha team,
team hizi zinakuwa zinamsupport msanii wao na kumpinga mpinzani wao.
Diamond
aliwahi kuhojiwa kwenye kipindi cha Sporah Show alisema, “Kuna wimbo wa
Alikiba ‘Singel Boy’ nilimuomba Alikiba kuingiza sauti tulipokuwa
studio alikataa na kusema kuwa nataka mteremko.”
Alikiba aliwahi kusema, “Kwenye
wimbo wa ‘Lala Salama’ niliingiza sauti yangu lakini nilishangaa kuona
sauti yangu imefutwa kwenye wimbo huo, kibaya zaidi ametumia melody
yangu niliyorekodia mwanzo.”
Hakuna
mwenye uhakika wa hili kuwa nani ni mkweli na nani anatudanganya.
Ugomvi wao unazidi kuwa mkubwa kila siku, sasa hivi umeenda mbali zaidi
mpaka msanii atakayekuwa karibu na mmoja kati ya hawa wawili wenye
ugomvi mwingine anakuwa anachukia.
Ukiwa
karibu na msanii mmoja unakosa support ya upande wa pili, hata kama
umeingia kwenye mashindano hutaweza kupigiwa kura na mashabiki wa team
nyingine. Hili linarudisha nyuma muziki wetu Angalia kilichotokea kwa
Ommy Dimpoz hutataka kuangalia tena nyuma, unakumbuka Wema Sepetu mwanzo
alikuwa team gani na sasa yuko wapi? Vipi Jokate kilichomtokea kwenye
pande zote mbili kwa sasa unadhani atakuwa wapi tena?
Angalia
support wanayopeana Wanigeria kwenye tuzo na muziki wao, hawaonyeshi
tofauti zao japo wapo wengi hawapatani. Kwanini tugombee fito wakati
tunajenga nyumba moja? Ni ukweli usihitaji ushahidi, Diamond akiingia
kwenye tuzo zozote mashabiki wa Alikiba hawampigii kura wanaona ni bora
kumpigia kura msanii wa nje ili Diamond akose hiyo tuzo.
Hilo
pia lipo kwa upande wa pili kama Alikiba akiingia kwenye mashabiki wa
Diamond hawampigii kura. Hata kama Wizkid ana ugomvi na Davido mashabiki
wao hawawezi kumpigia kura Diamond au Alikiba ili ashinde tuzo.
Kuna
haja wa kuweka tofauti pembeni na kuhakikisha muziki wetu unafika mbali
zaidi, ‘Kidole kimoja hakivunji chawa’, unajisikiaje tunaposhiriki
kwenye tuzo za nje kwenye category moja unawaona wapo wasanii wanne
kutoka Nigeria na mmoja tu ndiyo wa Tanzania.
Utajisikiaje
siku ukiona Jay Z akapenda kufanya kazi na msanii wa Tanzania? Kwa hili
lililopo sasa hivi kufika huko ni mbali sana, kila team inafanya msanii
mwingine asifanikiwa. ‘Adui muombee njaa’, kwetu imekuwa tofauti
tunaombeana wenyewe hiyo njaa.
No comments:
Post a Comment