Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli
alitoa orodha ya wakuu wapya wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara.
Katika orodha hiyo Rais Magufuli , amewaacha wakuu kadhaa akiwamo aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bwana Abbas Kandoro.
Kipindi cha Sun Rise cha Radio Times Fm, kimefanya mahojiano na Kandoro
asubuhi ya leo, ambapo amekiri kuachwa kwake na kuongeza kuwa tayari
amefikia kikomo cha uongozi kwa maana umri wake haumruhusu kuendelea
kutumikia nyadhifa hiyo.
“Unajua kuna watu wakituona wanajua kwamba bado tupo kwenye ujana, Ndugu
mtangazaji mimi nina miaka 66 sasa hivi, tayari umri umenitupa mkono
katika nafasi hii.
“Haijanishtua kwa sababu wakati tunapewa hii mikataba tuliambiwa kabisa
ukomo wa mkuu wa Wilaya ni miaka 60 na Ukuu wa Mkoa ni miaka 66, hivyo
nmetimiza umri wangu kisheria na napenda nimshukuru Mh Rais kwa hili”
Alisema Abbas Kandoro.
Mpaka kustaafu kwake, Kandoro amehodhi nafasi ya ukuu wa Mikoa katika
zaidi ya Mikoa Sita Tanzania Bara ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Singida
na Mbeya
March 14, 2016
Home
/
Unlabelled
/
Kauli Ya Abbas Kandoro Baada Ya Rais Magufuli Kukata Jina Lake na Kutomchagua Kuwa Mkuu wa Mkoa
Kauli Ya Abbas Kandoro Baada Ya Rais Magufuli Kukata Jina Lake na Kutomchagua Kuwa Mkuu wa Mkoa
Tags
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment