Watuhumiwa watatu wa kesi za ujangili pamoja na mauaji wametoroka
mahabusu katika kituo cha polisi wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, mara
baada ya kutolewa mahakamani kusikiliza kesi zinazowakabili.
Tukio hilo lilitokea terehe 19/02/2016 majira ya usiku, ambapo ilielezwa
kuwa walitoroka wakati mvua ikinyesha muda huo, huku wakichimba ukuta
kwa kutumia kitu chenye ncha kali kutoboa ukuta wa mahabusu hiyo.
Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi
Mkoani hapa Audax Majaliwa, alisema kuwa kutokana na tukio hilo askari
saba wanashikiliwa.
Majaliwa alisema kuwa watuhumiwa hao kabla ya kutenda tukio hilo, terehe
01/02/2016 walifikishwa katika mahakama ya wilaya ya Meatu ili
kusikiliza kesi zinazowakabili.
Aliwataja watuhumiwa hao waliotoroka kuwa ni Chiluli Sitta (28) mkazi wa
kijiji cha Mwasangula kata ya Itinje wilayani humo, ambaye alikuwa
akikabiliwa na kesi a mauaji.
Wengine ni Msanja Ndangule (45) pamoja na Paschal Masanja ambao ni Baba
na mtoto wake, wote wakazi wa kijiji cha Sapa kata ya Itinje wilayani
humo ambao walikuwa wakikabiliwa na kesi ya ujangili.
Alisema katika mahabusu hiyo walikuwemo jumla ya watuhumiwa sita, ambapo
watatu ndiyo walitoroka na wengine wawili walibaki, ambao ndiyo walitoa
taarifa kwa askari kuwa wenzao wametoroka kwa kuchimba ukuta.
“ jambo la kushangaza kwa nini wengine walibaki? Na hao waliotoroka
wanatoka kata moja…tunahofu hapa kuwa kulikuwepo na njama…lakini wale
waliobaki walieleza kuwa waliona dalili mapema kwa wenzao kuwa wako
kwenye mipango mikubwa” Alisema Majaliwa
February 25, 2016
Home
/
Unlabelled
/
Hili Hapa Ndio Tundu Lililochimbwa na Watuhumiwa wa Ujangili na Mauaji na Kufanikiwa Kutoroka Kama Al Chapo
Hili Hapa Ndio Tundu Lililochimbwa na Watuhumiwa wa Ujangili na Mauaji na Kufanikiwa Kutoroka Kama Al Chapo
Tags
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment