Wakati akikanusha vikali taarifa mbaya za kuzushiwa kifo mwishoni mwa
wiki iliyopita na watu ambao alisema hajui lengo lao, habari ya heri ni
kwamba, staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, (pichani)
anaelezwa kuwa kwenye shamrashamra za ndoa baada ya kudaiwa kulipiwa
mahari na mfanyabiashara maarufu jijini Dar (jina linahifadhiwa kwa
sasa).
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho ni mtu wa karibu wa Lulu, hivi
karibuni mrembo huyo alilipiwa mahari hayo kwa siri kwa kuwa mwanaume
huyo hakutaka mambo hayo yafike kwenye vyombo vya habari.
“Sasa mimi nawapa habari motomoto kuwa Lulu amelipiwa mahari na mwanaume
wake wa sasa lakini ishu nzima ilikuwa kwa siri sana,” kilidai chanzo
hicho na kuongeza:
“Shughuli nzima ilifanyika nyumbani kwa Lulu (Mbezi-Beach, Dar) na sasa
kinachoendelea ni taratibu za harusi lakini jamaa (huyo mwanaume) hataki
iwe na mbwembwe.
“Ndiyo maana Lulu sasa hivi ametulia siyo kawaida yake. Hata kwenye
viwanja vya bata na shughuli za mastaa haonekani kwa sababu anafanya
mazoezi ya kukaa nyumbani kama mke wa mtu.”
Habari hizo zilidai kwamba, Lulu ataolewa ‘soon’ kwani maandalizi
yamepamba moto kimyakimya chini ya usimamizi wa mama yake, Lucresia
Karugila.
Baada ya kunyaka madai hayo, Amani lilizungumza na Lulu ili kumpongeza
kwa kuchumbiwa na kulipiwa mahari kisha kusikia neno lake juu ya ishu
hiyo ambapo tofauti na matarajio ya mwanahabari wetu, msanii huyo
alikasirishwa na habari hizo huku akiweka wazi kuwa mambo mengine katika
maisha yake ni ya binafsi na kwamba siyo kila kitu anaweka wazi kwa
watu wengine.
“Hayo ni mambo binafsi, kwenye maisha yangu siyo kila kitu cha kuweka
wazi kwa watu,” alisema Lulu kisha akakata simu kwa hasira.
Chanzo:GPL
February 25, 2016
Hayawi Hayawi Sasa Yamekuwa....Mrembo Lulu Michael Adaiwa Kulipiwa Mahara...
Tags
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment