TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa (Pichani) anatumia majina matatu kama ifuatavyo: Kassim Majaliwa Majaliwa au Kassim M. Majaliwa.
Tangu
alipoteuliwa kushika wadhifa huo, kumekuwa na uchanganyaji wa majina
yake na hii ni kwa sababu tangu akiwa chuoni na jeshini, alikuwa
akitanguliza kutaja ubini (jina la ukoo) na ndiyo maana ikawa inasomeka
Majaliwa Kassim Majaliwa.
Endapo jina hilo litaanza kuandikwa na ubini, litapaswa kutenganishwa na koma kama ifuatavyo: Majaliwa, Kassim Majaliwa.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa aliteuliwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli
Novemba 19, 2015 na kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania siku hiyo hiyo. Aliapishwa Novemba 20, 2015 kwenye Ikulu ndogo
ya Chamwino, Dodoma.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATANO, DESEMBA 2, 2015.
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment