Mahakama
Kuu Kitengo cha Ardhi, imetoa hukumu kwa mfanyabiashara Marijani
Abubakar, almaarufu Papaa Msofe, Alex Massawe na Makongoro Nyerere kwa
kosa la kughushi hati ya umiliki wa nyumba iliyopo Mikocheni jijini Dar,
mali ya marehemu Onesphory Kituly aliyeuawa kwa kupigwa risasi na
majambazi mwaka 2011.
Kesi
hiyo iliyounguruma kwa takribani miaka saba tangu 2007, ilifikia tamati
Desemba 22, mwaka huu na kuwakuta na hatia washtakiwa hao baada ya
upande wa utetezi kushindwa kuwasilisha vielelezo vinavyowapa uhalali wa
kumiliki nyumba hiyo.
Akisoma
hukumu hiyo, jaji wa mahakama hiyo, John Nchimbi mbele ya wakili wa
Msofe na wenzake, Majura Maghafu alisema kuwa baada ya kupitia hoja
zilizowasilishwa na pande zote mbili, mahakama imeamua kumtangaza mke wa marehemu Onesphory, Mary Kituly kuwa mmiliki halali wa nyumba hiyo.
“Pia
mahakama imewatoza fani ya shilingi milioni 300, Papaa Msofe, Massawe
na Nyerere pamoja na asilimia 12 ya fedha hizo kama fidia ya gharama za
uendeshwaji wa kesi hiyo,” alisema Jaji Nchimbi.
Mara
baada ya kusomwa hukumu hiyo, mke wa marehemu, Mary aliangua kilio cha
furaha na nduguze mbele ya jaji baada ya kuona haki imetendeka, kitu
ambacho hakuwa akikitarajia.
“Yaani
siamini macho yangu, maana jinsi kesi ilivyonisumbua kwa miaka saba,
nimefarijika sana kwa haki kutendeka maana nilikuwa nikishindana na watu
wenye pesa, damu ya mume wangu haijapotea bure, namshukuru Mungu kwa
kweli,” alisema Mary alipokuwa akizungumza na waandishi ambapo alimshukuru pia Rais John Magufuli kwani serikali yake inajali haki.
Msofe
na wenzake walifunguliwa kesi katika mahakama hiyo mwaka 2007 baada ya
kudaiwa kughushi hati ya nyumba kwa kuhamisha umiliki wa nyumba namba
288 iliyopo Mikocheni, Dar iliyokuwa ya marehemu Kituly na kuweka jina
lake kisha kumuuzia Masawe kinyume cha sheria.
Ilidaiwa
kuwa kabla ya kufariki dunia, marehemu Kituly alimkopa shilingi milioni
30 Msofe kwa dhamana ya hati ya nyumba hiyo kwa makubaliano ya
kumrudishia kiasi hicho kwa muda wa miezi sita.
Inadaiwa
kuwa baada ya miezi mitano, marehemu alipata kiasi hicho cha fedha na
kurudisha kwa Msofe na kutaka hati yake, lakini alianza kuzungushwa
kuanzia kipindi hicho hadi alipokufa kwa kuuawa na watu wasiojulikana
mwaka 2011.
Oktoba 30, 2007, Msofe aliwatoa kwa nguvu marehemu, mke wake na watoto kwa madai kuwa nyumba hiyo imeuzwa kwa Massawe.
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment