Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto mbele)
akimsikiliza Mhandisi wa kituo cha kufua umeme wa dharura cha Kibeta-
Bukoba mjini, Mhandisi Filbert Mlaki wakati wa ziara yake kituoni hapo
leo (27 Desemba, 2015). Kituo hicho chenye mitambo minne kinao uwezo wa
kuzalisha megawati 2.1 ambacho hutumiwa pale umeme wa kutoka Uganda
unapokatika.
Serikali imesema ifikapo mwaka 2018 Mfumo wa umeme katika Mkoa wa Kagera utakua umeingizwa kwenye Gridi ya Taifa.
Hayo
yalisemwa jana tarehe 27 Desemba na Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo alipofanya ziara mjini Bukoba, Mkoani Kagera
ili kukagua miundombinu ya umeme.
Ilielezwa kwamba Mkoa huo kwa sasa
unapata umeme kutoka nchini Uganda ambao umekuwa ukikatika mara kwa mara
na hivyo kulilazimu Shirika la TANESCO kutumia mitambo yake inayotumia
mafuta ambayo hata hivyo haikidhi mahitaji ya umeme ya Mkoa.
Profesa
Muhongo aliliagiza shirika hilo kuhakikisha linaharakisha taratibu za
kuunganisha mkoa wa Kagera kwenye umeme wa Gridi ya Taifa.
"TANESCO
ni lazima muharakishe mipango ya kuunganisha mkoa huu kwenye gridi ya
taifa ili kuwapatia wananchi huduma ya umeme wa uhakika," aliagiza.
Aidha,
Profesa Muhongo aliiagiza TANESCO kuhakikisha mafuta kwa ajili ya
kuendeshea mitambo hiyo yanakuwepo yakutosha kwa muda wote.
Alisema
ifikapo mwaka 2025, Tanzania itaingia kwenye uchumi wa kati ambao
utatokana na uwekezaji mkubwa kwenye viwanda ambavyo vitahitaji umeme wa
kutosha na uhakika.
Mbali na hilo, Profesa Muhongo aliliagiza
Shirika la Tanesco mara baada ya mkataba uliopo wa kuuziana umeme kati
ya Tanzania na Uganda kuisha, wahakikishe wanaingia mkataba wa muda
mfupi mfupi lengo likiwa ni kuepusha kuwa ndani ya mkataba wakati tayari
mkoa huo utakua kwenye gridi ya taifa.
Akielezea hali ya umeme
mkoani humo, Meneja wa Tanesco Kanda ya Ziwa, Mhandisi Amos Maganga
alisema kwa sasa Tanzania inanunua umeme kwa gharama ya senti za
Marekani 8.4 kwa kila unit.
Alisema Tanzania inao mkataba wa
kununua umeme kutoka Uganda kiasi cha megawati 10 ambao unahudumia
wilaya za Bukoba Mjini na Vijijini, Karagwe, Muleba na Misenyi.(P.T)
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kushoto) akimsikiliza Mhandisi Filbert Mlaki.
Waziri wa nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akikagua moja ya mtambo wa kuzalisha umeme wa Kituo cha Kibeta
Moja ya mtambo wa kuzalisha umeme katika kituo cha kufua umeme wa dharura cha Kibeta- Bukoba Mjini.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella kabla ya kuanza ziara ya kukagua
miundombinu ya umeme mkoani humo.
December 29, 2015
Home
/
Unlabelled
/
Pamoja Kuwa na Kashfa ya Escrow Huyu Ndio Waziri Anayefanya Kazi Kuliko Mawaziri Wote wa John Pombe Magufuli....
Pamoja Kuwa na Kashfa ya Escrow Huyu Ndio Waziri Anayefanya Kazi Kuliko Mawaziri Wote wa John Pombe Magufuli....
Tags
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment