Nay wa Mitego amezungumzia jinsi alivyoachana na aliyekuwa mpenzi wake
Samsha Ford baada ya mwanadada huyo kudai hataki tena kutoka kimapenzi
na mastaa.
Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, rapa huyo alisema licha ya kuachana
na mwanadada huyo bado ni mshkaji wake na wanapiga stori kama kawaida.
“Mimi binafsi sijui alikuwa anamaanisha nini lakini kitu ambacho naweza
kusema mimi na Shamsa bado ni washkaji na hatuwezi kuja kuwa maadui hata
siku moja licha ya kuachana,” alisema. “Hatuna ugomvi lakini pia sijui
alikuwa na mahusiano na staa gani before? Labda ndiyo maana anaongea
hivyo ila mimi tuliachana vizuri.”
Aliongeza, “Kuhusu mimi sijamtenda hata yeye hajanitenda ndiyo maana
mpaka leo tunaendelea kuongea japo kuwa labda yeye ana kitu anacho
moyoni hicho siwezi kujua ila mimi ninachojua nazungumza naye poa tu.”
Kabla ya kuachana wawili hao walichukua muda mrefu kuweka wazi mahusiano yao.
December 30, 2015
Home
/
Unlabelled
/
Nay wa Mitego Afunguka Jinsi Walivyoachana Kimapenzi na Mwigizaji Shamsa Ford......
Nay wa Mitego Afunguka Jinsi Walivyoachana Kimapenzi na Mwigizaji Shamsa Ford......
Tags
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment