December 29, 2015

Mpekuzi blog Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, amejikuta akiangua kilio kama mtoto mdogo na kuwashangaza watu kufuatia mashabiki wake kumtaka awaimbie ‘akapela’ ya wimbo wake mpya wa Utanipenda. Tukio hilo ambao bado limo midomoni mwa mashabiki wake, lilijiri usiku wa kuamkia Boxing Day (Desemba 26, 2015) ndani ya ‘Uwanja wa Taifa wa Burudani’ Dar Live jijini Dar ambapo nyota huyo alikuwa akikamua jukwaani na shoo ya nguvu iliyopewa jina la Funga Mwaka Concert. Dakika chache kabla Diamond hajamwaga chozi, mashabiki wake walimuomba aimbe ‘akapela’ ya wimbo huo mpya. Wakati akiimba akapela hiyo, mashabiki wake, bila kificho, walimwambia anajitabiria ‘kufulia’ kwani wimbo huo una kila alama za yeye kumaliza gemu la Bongo Fleva vibaya. Hata hivyo, licha ya mashabiki kumpasulia hivyo, baadhi yao walianza kulia wakionekana kuguswa na mashairi ya wimbo huo hali iliyosababisha Diamond naye aanze kulia na kushindwa kuendelea kuuimba wimbo huo. Kufuatia hali hiyo, dada yake kwa upande wa baba yake, Abdul Jumaa, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ alimfuata jukwaani na kumtoa huku akimfunika na kitambaa cha bendera ya taifa ambacho pia dada huyo alikitumia kumfutia machozi kaka yake huyo. Diamond alipelekwa nyuma ya jukwaa ambako ukiachia mbali yeye Queen Darleen, meneja wake, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ naye alitumia nguvu ya ziada kumbembeleza staa huyo huku akimwambia anawapa wasiwasi mashabiki wake. Kwa hiyo anyamaze. Licha ya Babu Tale kutumia hekima ya kibabubabu, bado Diamond aliendelea kulia, safari hii kwa uchungu zaidi na kujiinamia huku akikataa kutulizwa wala kuambiwa maneno yoyote yanayoonekana ‘kama’ yana busara ndani yake. “Huna sababu ya kuendelea kulia ndugu yangu kwani kufulia au kuendelea kuwa na mali ni neema na msimamo wa Mungu. Hakuna binadamu anayeweza kumshusha mwenzake kama Mungu hajapanga kuwa hivyo,” alisema Babu Tale lakini Diamond hakumsikiliza. Diamond alinyamaza mwenyewe baadaye kufuatia mawasiliano ndani ya ubongo wake kumwambia ‘umelia sana kijana, imetosha sasa’! Kilio hicho, kilimaliza shoo hiyo kwani Diamond hakurudi tena jukwaani baada ya kukamua nyimbo zake kibao na kuwafanya mashabiki wake kuiweka siku hiyo katika kumbukumbu. Wimbo ulimuliiza Diamond huu hapa Mpekuzi blog Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana ) Newer Post Older Post Home What would Magufuli Do Habari Mpya Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya Disemba 29 Serikali Yasema Tamko Lake La Tiba Mbadala na Asilia Liko Palepale Zaidi ya Watu 1500 Wajitangaza Kuwa MASHOGA Mkoani Iringa Profesa Muhongo Azidi Kuibana TANESCO Wachimbaji Kadhaa Wafunikwa Na Kifusi Chunya, Mkoani Mbeye Leo Diamond Amwaga Machozi Ukumbini Yanga Yatangaza Kuvunja Mkataba Na Haruna Niyonzima....Yamtaka Kulipa Fidia ya Dola 71,175 Waziri Nape Akanusha Wizara Yake Kukataza Wanawake Kuvaa Mavazi ya Kubana Picha: Rais Magufuli Awaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri Waliokuwa Wamesalia Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya Disemba 28 HABARI MPYA Kali Zaidi No results HABARI MPYA Zilizosomwa Zaidi Picha: Lowassa Aanza Kuchunga Ng'ombe Kama Alivyoahidi Breaking News: Rais Magufuli amemalizia kuwateua Mawaziri Wanne Waliokuwa Wamebaki Gwajima Amkana Edward Lowassa.....Adai Yeye Hakuwahi Kumuunga Mkono Wakati Wa Kampeni Serikali Kuvunja Nyumba ya Waziri Mkuu wa Zamani Fredrick Sumaye. Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya Disemba 28 Familia Ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Yatoa TAMKO Zito....Yasisitiza Haihusiki na Utoroshaji wa Makontena Bandarini.Mwenye Ushahidi Autoe Kiama cha Wafanyakazi Waliosafiri Nje Ya Nchi chaja Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Disemba 27 Diamond Amwaga Machozi Ukumbini Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Disemba 24 My Blog List Latest Tweets Ungana Nasi Facebook Followers Blog Archive


Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, amejikuta akiangua kilio kama mtoto mdogo na kuwashangaza watu kufuatia mashabiki wake kumtaka awaimbie ‘akapela’ ya wimbo wake mpya wa Utanipenda.

Tukio hilo ambao bado limo midomoni mwa mashabiki wake, lilijiri usiku wa kuamkia Boxing Day (Desemba 26, 2015) ndani ya ‘Uwanja wa Taifa wa Burudani’ Dar Live jijini Dar ambapo nyota huyo alikuwa akikamua jukwaani na shoo ya nguvu iliyopewa jina la Funga Mwaka Concert.

Dakika chache kabla Diamond hajamwaga chozi, mashabiki wake walimuomba aimbe ‘akapela’ ya wimbo huo mpya.

Wakati akiimba akapela hiyo, mashabiki wake, bila kificho, walimwambia anajitabiria ‘kufulia’ kwani wimbo huo una kila alama za yeye kumaliza gemu la Bongo Fleva vibaya.

Hata hivyo, licha ya mashabiki kumpasulia hivyo, baadhi yao walianza kulia wakionekana kuguswa na mashairi ya wimbo huo hali iliyosababisha Diamond naye aanze kulia na kushindwa kuendelea kuuimba wimbo huo.

Kufuatia hali hiyo, dada yake kwa upande wa baba yake, Abdul Jumaa, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ alimfuata jukwaani na kumtoa huku akimfunika na kitambaa cha bendera ya taifa ambacho pia dada huyo alikitumia kumfutia machozi kaka yake huyo.

Diamond alipelekwa nyuma ya jukwaa ambako ukiachia mbali yeye Queen Darleen, meneja wake, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ naye alitumia nguvu ya ziada kumbembeleza staa huyo huku akimwambia anawapa wasiwasi mashabiki wake. Kwa hiyo anyamaze.

Licha ya Babu Tale kutumia hekima ya kibabubabu, bado Diamond aliendelea kulia, safari hii kwa uchungu zaidi na kujiinamia huku akikataa kutulizwa wala kuambiwa maneno yoyote yanayoonekana ‘kama’ yana busara ndani yake.

“Huna sababu ya kuendelea kulia ndugu yangu kwani kufulia au kuendelea kuwa na mali ni neema na msimamo wa Mungu. Hakuna binadamu anayeweza kumshusha mwenzake kama Mungu hajapanga kuwa hivyo,” alisema Babu Tale lakini Diamond hakumsikiliza.

Diamond alinyamaza mwenyewe baadaye kufuatia mawasiliano ndani ya ubongo wake kumwambia ‘umelia sana kijana, imetosha sasa’!

Kilio hicho, kilimaliza shoo hiyo kwani Diamond hakurudi tena jukwaani baada ya kukamua nyimbo zake kibao na kuwafanya mashabiki wake kuiweka siku hiyo katika kumbukumbu.

No comments:

Post a Comment