December 31, 2015

Kamanda Suleiman Kova Astaafu Rasmi Jeshi la Polisi Tanzania!

Leo ni siku ya mwisho kwa Kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova, kulitumika jeshi la Polisi nchini kwa kuwa muda wake wa kulifanyia kazi jeshi hilo umeisha.

Kamanda Kova ametoa taarifa hiyo leo asubuhi alipokuwa akizungumza katika kipindi cha kumekucha cha ITV, na kusema kuwa mkataba wake na jeshi la Polisi umeishia leo, hivyo analazimika kukaa pembeni.

"Mmepata bahati sana, maana wakati nakuja Dar es salaam mwaka 2008 nikitokea Mbeya, kwa mara ya kwanza nilifanya kipindi hapa na leo hii nawaagia hapa, leo ndio siku ya mwisho kwangu kulitumikia jeshi la Polisi, mkataba wangu na jeshi la Polisi unaisha leo, lakini siwaachi hivi hivi, Kaimu wangu yupo atakuwa nanyi", alisema Kamanda Kova.

Kamanda Kova alikuwa Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es salaam, na kwa mujibu wake amefanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa matukio ya kiuhalifu, yaliyokuwa yanaitikisa nchi hususani matukio ya wizi na uvamizi wa kwenye benki.

No comments:

Post a Comment