Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa amesifia kasi ya rais John Magufuli hasa katika kupambana na ufisadi nchini.
Dk. Slaa amesema kuwa alichowahi kukizungumzia awali kimetimia kwa kuwa nchi hii ilihitaji mtu kama Magufuli.
“Nadhani sasa unaelewa niliposhikilia msimamo wangu. Katika mazingira
ya sasa Magufuli ni bora zaidi. Niliwahi kusema kuwa hii nchi kwa siku
za mwanzo inahitaji udikteta kuirudisha kwenye mstari ulioonyooka,
nimefurahi sana,” Dk. Slaa ameliabia gazeti la Raia Mwema.
Amesema kuwa Bunge linatakiwa kufanya kazi ya kuudhibiti udikteta huo
ili usivuke mipaka lakini limuunge mkono kwa hatua anazochukua.
Katika hatua nyingine, Dk. Slaa amemshauri Rais Magufuli kuiangalia
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kuifumua.
“Pasipo kuchukua hatua ya kuifumua Takukuru, sina hakika kama matarajio yatafikiwa,” alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa hatua hizo zinapaswa kuchukuliwa haraka.
December 2, 2015
Home
/
Unlabelled
/
' Dk. Slaa Atoka Mafichoni 'Nadhani Sasa Mnanielewa Niliposhikilia Msimamo Wangu'
' Dk. Slaa Atoka Mafichoni 'Nadhani Sasa Mnanielewa Niliposhikilia Msimamo Wangu'
Tags
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment