KARIBU wapendwa wasomaji wa
safu hii. Nimeonelea siyo jambo baya nikiwadokolea mambo machache,
lakini muhimu ninayoyajua, ambayo yanasaidia sana kumhifadhi mume na
hivyo kuifanya ndoa yako kuwa imara kadiri siku zinavyokuja na
kuondoka.
Mojawapo ya jambo linalokosewa na wengi wetu ni aibu kwa waume zetu,
hasa tunapokuwa nao faragha. Hivi mtu unamuoneaje aibu mumeo chumbani
jamani, kwani ni nani wako yule, mjomba au mzazi?
Aibu hii ndiyo huwafanya wengine wawaache bila kuwasumbua waume zao,
kwa sababu tu wamekuja wamelewa au wamechelewa kuwasili nyumbani.
Nakwambia hivi, usithubutu kumuacha akalala wakati wewe unamhitaji,
utajikuta unaumiza nafsi yako bure, kwa nini uumie wakati wa kukupoza
yupo?
Fanya hivi
Mpokee vizuri na umchojoe nguo zake zote, kisha mpeleke bafuni uhakikishe ameoga, ukimaliza muulize kama atapata chochote cha kula, maana kuna wengine wakishapata kinywaji ni nadra kula, lakini pia mpeleke taratibu mpaka akubaliane na hali yako.

Kumbuka
Mume kulala na nguo hilo ni kosa lako mwanamke, unatakiwa kumpa mapokezi mumeo pale tu anapotoka kazini au kwenye mihangaiko yake popote bila kujali amerudi na nini au alienda kufanya nini.
Mume kulala na nguo hilo ni kosa lako mwanamke, unatakiwa kumpa mapokezi mumeo pale tu anapotoka kazini au kwenye mihangaiko yake popote bila kujali amerudi na nini au alienda kufanya nini.
Ukishamaliza sasa anza kumhangaisha kwa kumgusa sehemu unazohisi
zinaweza kumkumbusha nini unahitaji, katika hali ya kawaida, lazima
ataonesha ushirikiano. Na ikitokea ‘ameingia line’, acha aibu, onesha
uwezo wako kwa manjonjo yote unayojua.
Wanawake wengi wana aibu kuwaonesha waume zao mahaba, hasa kama
anamuhitaji eti atamuona ana uchu, hivi usipokuwa muwazi kwa mumeo,
unataka huo uwazi ukamuoneshe nani?
Shosti, usijali, jaribu kuwa mapepe kwa mumeo na awe mumeo tu uone,
kwa sababu wapo baadhi ya waume zetu wanatoka nje kwa sababu wanawake wa
nje ni mapepe, yaani wehu kabisa wawapo chumbani.
Utasikia mwanamke anasema mimi siwezi kumchojolea mume labda kuwe na
giza, nikwambie, wanaoiweza ndoa wote wakiwa ndani na wapenzi wao
wanajiachia vilivyo.
No comments:
Post a Comment