Serikali
imeamua kutoa elimu pasipo malipo kwa elimumsingi kuanzia elimu ya
awali hadi kidato cha nne,kuanzia mwaka wa masomo wa 2016.
Azima
hii ya serikali ni katika kutekeleza sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka
2014 ambayo ina lengo la kuhakikisha kwamba watoto wote wa Tanzania
wanapata Elimu bila kikwazo ikiwemo ada au malipo.
Katika
kutekeleza maamuzi hayo,ada zote zilizokuwa zikilipwa kwa ajili ya
elimu ya kidato cha kwanza hadi cha nne zimefutwa.Pia, waraka wa Elimu
namba 8 wa mwaka 2011 kuhusu michango shuleni nao pia umefutwa.
Aidha,
mwongozo wa elimumsingi bila malipo unaandaliwa na utatumwa kwa
wamiliki wa shule ifikapo au kabla ya tarehe 15 Disemba 2015.
Waraka huu umeanza kutumika tarehe 21 Novemba 2015
No comments:
Post a Comment