
RIP Mchungaji Christopher Mtikila… Asubuhi ya Octoba 4, 2015 taarifa ya Majonzi ilitufikia ambapo taarifa yenyewe ilikuwa inahusu msiba wa aliyekuwa Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa chama cha kisiasa cha DP Christopher Mtikila amefariki kwa ajali ya gari wakati akitokea Morogoro kuelekea Dar es salaam.
Mwili wa Marehemu umeagwa leo October 7,2015 kuelekea mkoani Njombe na watu mbalimbali wamejitokeza kuaga mwili wa Marehemu katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam wakiwemo viongozi wa Serikalini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wwa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal ni miongoni waliouwaga mwili wa marehemu Christopher Mtikila wa DP.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad ni miongoni mwa waliouwaga mwili wa marehemu Christopher Mtikila wa DP katika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam.






















No comments:
Post a Comment