Rhoda Chegele akiwa na uvimbe kichwani unaomsababishia maumivu makali.
Rhoda ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jengo la
Mwaisela, Wodi Namba 2 akiwa ametokea mkoani Kilimanjaro, Wilaya ya
Same, Mtaa wa Bomani alitembelewa na waandishi wetu mwishoni mwa wiki
iliyopita hospitali hapo ambapo alikuwa na haya ya kusema:ANA MAGONJWA MENGI
“Nimeshahangaika katika hospitali mbalimbali lakini hali yangu inazidi kuwa mbaya kila kukicha, nahofia maisha yangu kwa sasa kwani ninakabiliwa na magonjwa mengi ukiwemo wa goita na huu uvimbe ambao umekuwa na maumivu makali, sipati usingizi, kila wakati ni kuhangaika hospitali.
“Hapa nilipo zinahitajika fedha zaidi ya shilingi milioni moja kwa ajili ya vipimo na upasuaji, sina lakini kinachoniumiza sana ni pale wanangu wanaosoma wanaponiambia niwapatie fedha za matumizi shuleni huku nikiwa katika hali mbaya kupita kiasi.
CHANZO CHA UGONJWA
“Sikumbuki ni tarehe ngapi nilianza kuumwa ila ninachokijua ni zaidi ya mwaka mmoja, ulianza kama uvimbe katika paji la uso, nikawa naenda hospitali kutibiwa sikuona mabadiliko, nilikwenda hadi hospitali ya wilaya yetu ya Same lakini hakukuwa na unafuu, niliamua kwenda Hospitali ya Kibosho, Moshi.
“Huko nilifanyiwa vipimo ambapo walisema wanaweza kunifanyia upasuaji wa goita lakini kila walipopanga muda wa kunifanyia presha ikawa inapanda, wakanishauri niende Hospitali ya KCMC ambapo vipimo vilifanyika walinipa dawa lakini hakukuwa na mabadiliko.
KUHAMIA MUHIMBILI
“Niliwaomba niletwe Muhimbili ambapo nilifika hapa Mei mwaka huu, walifanya vipimo kuangalia kama kuna ugonjwa wa kansa lakini walibaini ni goita na uvimbe ingawa bado wanaendelea na uchunguzi, nipo katika mtihani mgumu sana, sijajua ni lini nitafanyiwa upasuaji.
“Ama kweli sura ya binadanu inaweza kubadilika kwa dakika chache, nimeamini kwani mimi leo hii nashindwa hata kwenda kanisani, nakumbuka kuna kipindi nilikuwa nikienda nikiwa mgonjwa lakini watoto walikuwa wakinishangaa, wakawa wananifuata nyuma huku wakinipa pole.
“Naomba msaada. Nimelazimika kuwapa wananchi kilio changu ili waweze kunisaidia maana matibabu yangu yanahitaji fedha nyingi ambazo sina, mimi ni wa kitandani tu. Yeyote aliyeguswa na maradhi yanayonitesa anaweza kunisaidia kwa kupitia namba yangu ambayo ni O755 O80683,” alisema mama huyo.
No comments:
Post a Comment