Dr. Slaa: Uchaguzi huu ni wa kipekee. Watanzania wanataka mabadiliko. Umma haujatafsiri maana ya mabadiliko
Dr. Slaa: Dhana ya mabadiliko haijaelewa vyema. Dhana hii si mpya. Ilisemwa hata na Hayati Mwalimu Nyerere
Dr. Slaa: Mabadiliko yana sura mbili. Yapo ya kutoka pazuri
kwenda kubaya na ile ya kutoka kubaya kwenda kuzuri. Anatoa mfano wa
Dikteta Benito Mussolin wa Italia
Dr. Slaa: Ninahisi tafsiri ya mabadiliko haijaeleweka. Hata
wasomi hawaelewi. Kwa upande wa wenzetu wapinzani wanachukua mifano ya
hata Marekani ambapo Obama alikuwa na sifa..
Dr. Slaa: Msingi wa mabadiliko ni kutoka ulipo kwenda mahali
kwingine. Kwenda kuzuri. Kuna dhana ya mabadiliko na mapinduzi. Kuna
kauli za kutishia kuingia barabarani
Dr. Slaa: Wapo wenye tamaa ya kwenda Ikulu. Hiyo si ambition ya uongozi. Ambition inaambatana na maandalizi
Dr. Slaa: Kumchagua Rais si suala dogo. Tutavumilia kwa miaka mitano
Dr. Slaa: Amani inapaswa kuwa ajenda kuu kwakuwa ni zao la demokrasia.
Dr. Slaa: Naungana na Jaji Warioba kuwa rushwa ilikuwa inatisha.
Serikali za Mitaa hupewa asilimia 23 za bajeti. Asilimia 75 ya 23
hupotea kwa rushwa. Kuna grand na petty corruption. Rushwa ndogo huumiza
kuliko kubwa kwakuwa zinagusa watu wanyonge.
Dr. Slaa: Katika kampeni za mwaka huu,chama changu CHADEMA
kimeacha ajenda ya rushwa. Hata nyimbo za hamasa za kupinga rushwa
hazisikiki. ACT ni kama wanairithi CHADEMA kwenye ajenda ya rushwa.
Nampongeza Zitto na chama chake. Yuko committed
Dr. Slaa: Msingi wa mabadiliko ni kutoka ulipo kwenda mahali
kwingine. Kwenda kuzuri. Kuna dhana ya mabadiliko na mapinduzi. Kuna
kauli za kutishia kuingia barabarani
Dr. Slaa: Dr. Magufuli anasisitiza kuwa anapiga vita rushwa.
Sijaona jambo hilo kwa CHADEMA. Ukiwa mchafu huwezi kukemea. Dr.
Magufuli anasema ataanzisha Mahakama Maalum za rushwa na ukimtazama
anaaminika. Dr. Magufuli sijawahi kusema ni msafi. Lakini ana nafuu kati
ya wagombea nane
Dr. Slaa: Tulimpinga Rais Kikwete mwaka 2010 kuwanyanyua
Mramba,Chenge na Lowassa. Magufuli haogopi kupoteza kura kwa kukemea
ufisadi na kusema atawafunga wala rushwa. Magufuli ni jasiri
Dr. Slaa: Kuna michakato inafanyika kama kuwaleta na malori na
mabasi. Chama changu kilikuwa hakibebi watu. Lakini kilibeba kwenye
mkutano wa Jangwani.
Dr. Slaa: Baada ya kusikiliza na kuona mikutano,kwanza tujiulize
tunataka Rais wa aina gani. Mwenye vigezo vya kupambana na rushwa,
Magufuli anafaa. Rais hawezi kuongea kwa dakika kumi, nani atakuwa Rais?
Ni akina Sumaye?

No comments:
Post a Comment