October 12, 2015

Lowassa: Wananchi Anzeni Kusherekea na Kushangilia Ushindi

Huku zikiwa zimebaki siku 13, Mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendelea na anayeungwa mkono na umoja wa Ukawa Ndg. Edward Lowassa kawataka wananchi waanze sasa kushangilia ushindi na ukombozi wa pili wa Taifa hili.

Lowassa kasema hayo jana alipokuwa mjini Musoma, ambapo alipata mapokezi ambayo hayajawahi kutokea, tokea nchi ipate uhuru. Lowassa kasema kutokana na mapokezi na hamasa kubwa ya vijana, wakina mama, na wazee anayopata, kawataka wananchi waanze kushangilia ukombozi wa pili unaotarajiwa kutokea oktoba 25.

Lowassa kasema baada ya oktoba 25, kila mwananchi ataanza kufaidika na matunda ya mgao wa keki ya Taifa, na sio hali ilivyo ya sasa, ambapo keki inamegwa na wachache na kuacha vijana wengi, bodaboda, machinga, wakina mama vijijini, walimu, madaktari, wafanyabiashara, wauguzi, wakulima na wafugaji wakiwa hawana hata uwakika wa kupata milo mitatu. Hilo linakoma mara moja baada ya oktoba 25..

"najua uhuzi, masikitiko na mfadhaiko mliyonayo wananchi. Mwisho wa hayo yote ni tarehe 25, ndio maana nataka muanze kusherekea kuanzia sasa kwani naenda kuwatoa kwenye kifungo cha kunyimwa fursa na serikali ya CCM kwa zaidi ya miaka 54"...

Vile vile kawataka wananchi kwa uwingi wao siku ya tarehe 25.10.2015 wajitokeze kwa wingi sana sana kupiga kura...

No comments:

Post a Comment