October 6, 2015

Habari ya Waziri Abdalah Kigoda Kufariki zilizoenea Kwenye Mitandao ya Kijamii..Huu Hapa Ukweli

Afya ya Waziri wa viwanda na biashara, Abdallah Kigoda inaendelea kuimarika akiwa anapatiwa matibabu nchini India na hajafariki kama habari zilivyosambazwa kwenye mitandao.
Kaka wa Waziri Kigoda anayefahamika kwa jina la Sadick amekanusha habari zilizoenea kuwa Waziri Kigoda amefariki ambapo amesema kuwa Mh. huyo anaendelea kupatiwa matibabu ya figo na hali yake kwasasa ni bora kuliko wakati anapelekwa.
" Nimepokea simu zaidi ya 60 zikinipa pole ya kuwa tumefiwa, nikaamua kuwasiliana na dada yetu ambaye yuko na mgonjwa nchini India na amenithibitishia kuwa Mh. Abdallah Kigoda ni mzima na afya yake inazidi kuimarika" amesema kaka wa Waziri Kigoda

No comments:

Post a Comment