October 11, 2015

Diamond, Vanessa Mdee na Ommy Dimpoz washinda tuzo za Afrimma

Diamond Platnumz ameibuka na ushindi mkubwa zaidi kwenye tuzo za Afrimma zilizofanyika Dallas, Marekani alfajiri ya leo kwa saa za Afrika Mashariki.

Diamond Plutnumz ndiye msanii aliyekomba tuzo nyingi mwaka huu kwa kubeba 3 ambazo ni Video bora ya kucheza NANA, Msanii bora wa Afrika Mashariki na msanii wa mwaka.

Vanessa Mdee amechukua tuzo ya msanii bora wa kike Africa Mashariki.

Ommy Dimpoz ameondoka na tuzo ya msanii bora anayechipukia.

No comments:

Post a Comment