September 12, 2015

SIKIA KAULI YA ESTER BULAYA BAADA YA POLISI KUVAMIA HOTEL ALIYOSHUKIA NA KUMPEKUA

Akizungumzia hali hiyo, Bulaya ambaye alifikia hoteli hiyo kwa lengo la kuendelea na mikutano yake ya kampeni, alidai kuwa askari hao kufanya upekuzi huo ni njama za CCM za kutaka kumkatisha tamaa na kwamba hawataweza.
Amesema wananchi wa Bunda wameishaichoka CCM na rangi zao na makopo yao (wagombea wao) hivyo ndiyo maana wanatumia mbinu hizo ili kuwakatisha tamaa na kamwe mbinu hizo hazitafanikiwa, kumrudisha nyuma katika harakati za kulikomboa Taifa.
Hata hivyo Bulaya hivi karibuni alichukuliwa na jeshi la Polisi wilayani humo kwenda kumhoji, mara baada ya kutoka amesema Mkuu wa Polisi Wilaya OCD, alionekana akipendelea upande mmoja wa CCM.
Bulaya ambaye anaoeneka kuungwa mkono na wananchi wa jimbo hilo hususani vijana na wanawake, amekuwa akimshambulia waziri wa Kilimo na Ushirika, Steven Wassira kwa kushindwa kuwatatulia kero zao, hiyo ndiyo inaelezwa kuwa chanzo za kufanyiwa fitina hizo.
Akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kung`ombe na kuhudhuliwa na mamia ya wananchi, amesema Wassira ameshindwa kuwaletea maendeleo wananchi wa Bunda, ikiwemo tatizo la maji ambalo limekuwa `sugu` jimboni humo

No comments:

Post a Comment