September 4, 2015

NAFASI ZA KAZI.NAFASI ZA KAZI ...SEREKALINI CHECK HAPA NAFASI KIBAO ZA KAZI SEREKALINI LEO

OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA YA HANDENI
KUMB: Na. HW/S.20/96/1

TANGAZO LA NAFASI ZA JAZI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni anawatangazia wananchi wote Raia wa Tanzania wenye sifa zinazohitajika kuomba kujaza nafasi wazi za kazi mbalimbali kama ifuatavyo:-
1. KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III- (NAFASI 4)
SIFA/ELIMU/UJUZI
Kuajiliwa wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria mafunzo ya uhazili na kufaulu mtihani wa hatua ya tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika program za windows, Microsoft Office, Excel, Internet, E-mail na Publisher.
NGAZI YA MSHAHARA
Cheo cha katibu Mahsusi Daraja la III kina ngazi ya mshahara wa TGS B
KAZI NA MAJUKUMU YA KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III
i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida
ii. Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa
iii. Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi na kumuarifu mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
iv. Kusaidia kutafuta na kumpatia mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
v. Kusaidia kufikisha maelekezo ya mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
vi. Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa maofisa walio katika sehemu alipo, kukusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
vii. Kutekeleza kazi zozote atakazokuea amepangiwa na msimamizi wake wa kazi.
================

2. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – (NAFASI 2)
SIFA/ELIMU/UJUZI
Mwombaji awe amehitimu kidato cha nne au sita na awe ametunukiwa cheti cha Utunzaji Kumbukumbu katika mojawapo ya Fani za Afya, Masijala, Mahakama na Ardhi.
NGAZI YA MSHAHARA
Cheo cha Msaidizi wa Kumbukumbu kina ngazi ya mshahara ya TGS B
MAJUKUMU NA KAZI ZA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II
i. Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajika na wasomaji.
ii. Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.
iii. Kuchambua kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
iv. Kuweka/kupanga kumbukumbu katika reki (file racks/cabinets) katika masijala/vyumba vya kutunzia kumbukumbu.
v. Kuweka kumbukumbu (barua/nyaraka nk) katika mafaili.
===============

3. DEREVA DARAJA LA II – (NAFASI 2)
SIFA/ELIMU/UJUZI
Mwombaji awe amehitimu kidato cha nne au sita mwenye Leseni Dalaja la “C” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu (3) bila kusababisha ajali, mwenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la II (Trade Test Certificate Grade Two)
MSHAHARA
Cheo cha Dereva Daraja la II kina ngazi ya mshahara wa TGOS A
MAJUKUMU NA KAZI ZA DEREVA DARAJA LA II
i. Kuendesha magari ya abiria na malori
ii. Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote na kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo
iii. Kufanya matengenezo madogo katika gari
iv. Kutunza na kuandika daftari la safari “log-book” kwa safari zote

MASHARTI YA JUMLA KWA NAFASI ZOTE
i. Mwombaji awe Mtanzania mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45
ii. Barua za maombi ziandikwe kwa mkono na kutumwa kwa anuani iliyotajwa hapo chini
iii. Mwombaji aambatanishe nakala za vyeti vya taaluma, cheti cha kuzaliwa maelezo binafsi (CV) na nyaraka zote muhimu pamoja na pich (passport size) mbili (2) zilizopigwa hivi karibuni
iv. Kwa wale watakaopita kwenye mchujo wa awali (short listed candidates) ndio watakaoitwa kufika kwenye mahojiano (interview) na watatakewa kufika na nakala halisi za vyeti husika.
v. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha kutozingatia hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa BATILI.
vi. Barua zote zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni
S.L.P.355
HANDENI

Aidha uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za halmashauri HAURUHUSIWI.
mwisho wa kupokea maombi 16/9/2015
LUIZA O. MLELWA
MKURUGENZI MTENDAJI (H/W)
HANDENI.

Source: Habari Leo 2nd September, 2015

No comments:

Post a Comment